Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo: George Nyatongo
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu
nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi
3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) Agosti 10 na 12,
2012 zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari
mbalimbali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649
ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo ya
vyuo.
Miongoni mwa makosa ama dosari
ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa
vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa
picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali
za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.
Kwa upande wake TCU imewaengua
jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha
katika taarifa yake.
Miongoni mwa dosari ambazo
zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za
vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O’ level na A’ level Index
number), miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa
muombaji (Contact information e.g. Mobile phone number, email address and
postal address) pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).
Waweza kuingia katika linki hii
hapo chini na kuona majina ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika maombi
yao kwa TCU
Pia waweza kutembelea linki
zifuatazo na kushuhudia majina ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika
maombi yao kwa bodi ya mikopo;-
http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=365&Itemid=66 http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=366&Itemid=67 http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=367&Itemid=68
Post graduate;-
Hata hivyo taasisi hizo mbili
zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na
kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa
taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz na www.tcu.go.tz
Habari hii imeandaliwa na
mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
No comments:
Post a Comment