To Chat with me click here

Thursday, August 23, 2012

MSHINDI WA BIBI BOMBA 2012 NI VERONICA MPANGALA AKA “TUKINAAA”!


Bibi Veronica Mpangala akikabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh mil 5 baada kuwa mshindi wa kwanza.
Bibi Veronica Mpangala akiwa na baadhi ya waandaaji wa shindano la Bibi Bomba katika picha ya pamoja.

Bibi Veronica Mpangala akikabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh mil 5 baada kuwa mshindi wa kwanza. Lile shindano la Bibi Bomba lilokuwa likiendeshwa na Clouds TV limefikia kilele chake dakika chache zilizopita na Bibi Veronica Mpangala kuibuka mshindi kwa kuwazidi wenzake kwa mbali sana kama graph inavyoonesha kwenye picha zinazo endelea. Bi Veronica amejishindia Tsh 5,000,000/= pamoja na zawadi nyingine. Nafasi ya pili imeshikwa na Anna Said a.k.a Mzee wa Dongo na kupata Tsh. 3,000,000/= wakati nafasi ya tatu ikishikwa na Bi. Nasra Mohamed ambaye ameshinda Tsh. 1,500,000. Washiriki wengine walioingia kwenye 8 bora walijipatia zawadi ambazo hazikutajwa.


Ona Bibi Veronica alivyo wakimbiza washiriki wenzake
 Huyu ni mshindi wa pili Bibi Anna Said a.k.a Mzee wa Dongo aliye jishindia Tsh 3,000,000
Nasra Mohamed, mshindi wa tatu wa Bibi Bomba alikabidhiwa mfano wa hundi wa sh. 1,500,000/


 Mabibi waliotoka katika shindano hilo la Bibi Bomba katika hatua ya kwanza wakikabidhiwa zawadi zao za kushiriki shindano hilo. 
Sehemu ambapo Mabibi Bomba walikuwa wametayarishiwa katika hafla hiyo ya kumtangaza mshindi wa shindano hilo. 
Wadau na waandaji wa Bibi Bomba wakiwa katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment