KATIBU
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni
iliyoko ndani ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), cha Mikumi wilayani Kilosa,
Mkoa wa Morogoro kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni sababu za kisiasa.
Tukio
hilo lililoambatana na kuzimwa kwa umeme katika mji mdogo wa Mikumi na
vitongoji vyake kwa siku nzima, limetafsiriwa na Dk Slaa kuwa ni hila
zinazofanywa na CCM kuhujumu operesheni ya Chadema ya Vuguvugu la Mabadiliko
(M4C) inayoendelea katika wilaya mbalimbali mkoani humo.
Dk
Slaa aliwasili chuoni hapo majira ya saa 8.00 mchana akitokea wilayani Ulanga
katika Operesheni M4C ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni Sangara iliyofanyika
katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Baada
ya kuwasili katika hoteli ya chuo hicho, Dk Slaa alipokewa na wahudumu wa
hoteli hiyo na kukabidhiwa funguo ya chumba namba tano ambacho Mkurugenzi wa
Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Rwakatare, alikiomba kwa
ajili yake.
Muda
mfupi baada ya kuchukua funguo hizo, akatokea meneja wa hoteli hiyo ambaye jina
lake halikufahamika mara moja na kumweleza Dk Slaa kuwa sehemu hiyo
imeshawekewa ‘booking’ hivyo Dk Slaa aondoke.
Tukio
hilo lilimfanya Dk Slaa ahoji mantiki ya hatua hiyo hasa, baada ya mhudumu wa
hoteli hiyo kumkubali na kukabidhi funguo kwake na meneja huyo kumnyang'anya
funguo hiyo.
Funguo
ya chumba alichotakiwa afikie Dk Slaa alikabidhiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa Chadema, Rwakatare baada ya kukiomba chumba hicho siku kadhaa nyuma.
Hata
hivyo, meneja huyo alisisitiza Dk Slaa kuondoka kwa kuwa yeye hakuwa na taarifa
na ujio wake.
Kufuatia tukio hilo Dk Slaa aliondoka na kuelekea katika eneo la mkutano wa hadhara ambako pia umeme ulizimwa ghafla hivyo, kuongozea hisia kwa Dk Slaa kuwa alikuwa anahujumiwa kwa kuwa hakukuwa na ratiba ya mgawo wa umeme siku hiyo.
Akizungumza
katika mkutano wake huo, Dk Slaa alikituhumu CCM kuwa ndiyo kilichoandaa mpango
huo kwa lengo la kuhujumu kampeni zake za kumkomboa Mtanzania.
Hata
hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipuuza madai hayo ya
Dk Slaa akisema, "Namshauri aache siasa kwa kuwa zimeanza kumshinda,"
Nape
alisema Dk Slaa hawezi kueleweka kukihusisha CCM na kufukuzwa kwake hotelini
kwani hoteli hiyo ya Veta, siyo mali ya chama hicho tawala.
"Dk
Slaa amezeeka. Aache siasa awaachie vijana. Yeye afukuzwe huko halafu aseme CCM
tunamhujumu! Namshauri apumzike siasa awaachie vijana waendeleze
gurudumu," alisema Nape.
Meneja
wa Tanesco, Mkoa wa Morogoro, Deogratius Ndamugaba, akijibu shutuma za kukatika
kwa umeme katika mji huo alisema kuwa kukatika huko kulitokana na hitilafu za
kawaida na siyo hujuma au msukumo wa kisiasa.
“Kukatika
kwa umeme Mikumi si kwa sababu ya Chadema ila ni feeder ya Mikumi iko nje tangu
saa 12.45 jioni, nguzo imeanguka na inapaswa kubadilishwa na sehemu yenyewe ni
porini, kuna giza na chui,” alisema meneja huyo.
Slaa amvaa Nape
Katika hatua nyingine, Chadema kimemtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kutoa elimu kwa viongozi wa chama hicho tawala kuzungumza kwa busara mbele ya wananchi kwani kinyume chake wanamletea sifa mbaya.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara ya chama hicho katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, Dk Slaa alisema kuwa ni kawaida ya mtu mwenye tabia mbaya kama vile mwizi kujishtukia na kufikiria kuwa hata wenzake ni wezi.
Alisema kuwa ni aibu kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuachia viongozi walio chini yake ndani ya chama hicho kutoa matamko yanayoivua nguo Serikali kuwa haiko makini na inazidi kukupoteza dira na mwelekeo wake.
“Nataka nimalizie na suala moja ambalo limetokea leo mchana. Kuna tamko moja limetolewa na kijana mmoja wa CCM anaitwa Nape, sasa kwa sababu ni kama kinda la njiwa kwangu, sitamjibu yeye. Alichokisema kwa watu wanaojua, tunamshangaa Kikwete kwa kuachia mambo ya chama chao na Serikali yake kwa jumla.

No comments:
Post a Comment