TAKUKURU YADAI
ALIKUWA AKIGAWA FEDHA
Mhe. Mussa Azzan Zungu |
WINGU
la rushwa limeendelea kutanda katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), na sasa Mbunge
wake wa Ilala, Mussa Zungu, anashilikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), akituhumiwa kutoa rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya
Wazazi.
Zungu
ambaye anakuwa mbunge wa pili wa CCM kunaswa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa,
anashikiliwa pamoja na wajumbe wawili wa jumuiya hiyo.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge, alikuwa akigombea nafasi ya Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) kupitia Jumuiya ya Wazazi
Tanzania Bara na alinaswa juzi sambamba na Dk. Damas Mukasa na Fatuma Kasenga.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa
Dodoma, Yunis Munisi, alisema Zungu alikamatwa Oktoba 30, mwaka
huu, siku moja kabla ya uchaguzi huo.
Akielezea
mazingira ya kukamatwa kwao, alisema Zungu alikamatwa akiwa na wapambe wake
wanne akitoa rushwa kwa wajumbe ili wampigie kura.
Kuhusu
Dk. Mukasa ambaye alikuwa akigombea nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Wazazi
Taifa na mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Munisi alisema
alikamatwa Oktoba 8, mwaka huu, nje ya Ukumbi wa Kilimani mjini hapa kwa
kosa la kutoa rushwa kwa wajumbe ili wampigie kura.
Pamoja
na hilo, wajumbe wengine wawili nao wanashikiliwa na TAKUKURU kwa kosa la
kupokea rushwa kutoka kwa Dk. Mukasa ili wamchague.
Mgombea
mwingine aliyekamatwa, Fatuma, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa
wa Mbeya na Mkutano Mkuu Wazazi Taifa, alikamatwa saa tisa usiku wa kuamkia
jana akiwa analipia baadhi ya wajumbe wa mkutano vyakula na vinywaji.
“Inaaminika
kwamba huo ulikuwa ni ushawishi ili wajumbe wamchague...alikamatwa katika
nyumba ya wageni ya Kitoli iliyopo eneo la Iringa Road mjini Dodoma,” alisema
Munisi.
Alisema
TAKUKURU imekuwa ikifuatilia taarifa za vitendo vya rushwa tangu kuanza kwa
chaguzi za ndani za CCM kuanzia ngazi za chini hadi taifa kwa lengo la
kuzuia na kupambana na vitendo hivyo.
Munisi
alisema hatua hiyo imefanikiwa kuzuia vitendo vingi ambavyo vilitaka
kutendeka baada ya kupata mipango hiyo na kuitibua kabla ya kufanikiwa.
Hata
hivyo, alisema changamoto kubwa waliyokumbana nayo ni kitendo cha wajumbe
kushirikiana na wagombea na wapambe wao katika vitendo vya rushwa, na hivyo
kuwa shida kufanya ushirikiano.
Alisema
changamoto nyingine inatokana na wananchi kudai wameona vitendo vya rushwa
vikitendeka, lakini hawachukui hatua zozote za kutoa taarifa TAKUKURU.
Kuhusu
tuhuma zinazowakabili akina Zungu na wenzake, alisema uchunguzi unaendelea.
No comments:
Post a Comment