To Chat with me click here

Wednesday, October 31, 2012

HIVI NDIVYO MOSHI ILIVYO LEO!!!

 Baadhi ya Maeneo ya Mji wa Moshi kama yaonekanavyo yalivyo masafi.
Haya ni maeneo ya Stendi Kuu ya Mabasi-pamoja na kuwa na pirikapirika nyingi lakini bado usafi ni wahi ya juu

Moshi ni moja kati ya miji misafi katika Afrika ya Mashariki, usafi wa mji huu wa Moshi umekuwa ukiibua mjadala na maswali mengi sana kichani kwangu na kwa baadhi ya watanzania wenye kudadisi mambo. 

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuutembelea huu mji katika moja ya shughuli zangu, na nilipokuwa nikipita katika baadhi ya maeneo ya mji huo, kwakweli nilishuhudia ni jinsi gani wakaazi wa manispaa hiyo walivyojidhatiti katika kuhakikisha waufanya mji wao kuwa msafi na mfano wa kuigwa katika Tanzania yetu na hata nje ya mipaka yake. 

Maswali mengi ambayo nimekuwa nikijiuliza ni kuwa; 
  1. Hivi watanzania wa mikoa mingine hususani Dar-Es-Salaam, hawaoni umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi wa jiji kama ilivyo kwa manispaa ya moshi? 
  2. Je watu hawa wa moshi si watanzania kama sisi wa mikoa na sehemu nyingine za Tanzania? 
  3. Kama ndivyo je ni kwanini tumekuwa na utofauti wa kiutashi katika kujali na kutumnza mazingira? 
  4. Vipi kuhusu viongozi wa halmashauri nyinginezo pamoja na serikali kuu? Je hazipaswi kuiga mfano wa manispaa ya moshi, viongozi wetu hususani wa hapa Dar, wamekuwa wakipigapiga maneno tuu juu ya utunzwaji wa mazingira lakini hakuna hatua thabiti zinazochukuliwa pale watu wanapothibitika kuvunja sheria nyingi za kimazingira. 
  5. Pia kwa dhana hii ya uchafu uliokithiri katika miji na vitongoji vyetu, je tunaweza kutekeleza kwa dhati azimio la serikali la kupambana na magonjwa ya milipuko kama maralia, kipindupindu n.k ? 
Maoni yangu: 

Kwanza kwa dhati ya moyo wangu napenda kuwapongeza sana viongozi wa manispaa ya Moshi kwa kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha utekelezwaji wa mipango na malengo yao ya kuifanya moshi kuwa mfano wa kuigwa kiusafi. 

Napenda pia kuwashukuru wananchi wa Manispaa hiyo ya Moshi kwa kuwa waelewa na wenye kutambua umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi wa mji wao kiasi ya kuupa heshima kubwa katika Tanzania yetu na kuwa mfano wa kuigwa. Ninawapongeza sana kwa utiifu wa sheria zao na kwa kuzitekeleza bila shuruti. 

Nawaasa viongozi wa halmashauri na manispaa nyinginezo; kuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali ambazo zitasaidia kutoa hamasa kwa wananchi wao kudumisha usafi wa mazingira yetu kwam ilivyo moshi. 

Viongozi hawa, pia wao wenyewe wawe ni mfano bora wa kuigwa katika kutekeleza maazimio ya kimazingira. Wawe tayari kusimamia na kuwajibika pia kuwawajibisha wahusika wote ambao ni kikwazo kwa kufikia au kutekeleza malengo mazuri ya kudumisha usafi wa mazingira yetu katika halmashauri zetu. 

Wananchi wote kwa ujumla, tunapaswa kuelewa kuwa usafi ni moja ya njia muhimu za kupunguza ugumu wa maisha haswa kwa sisi wananchi wenye kipato cha chini. Tukumbuke kuwa magonjwa mengi hutokana na uchafu, haya magonjwa huongeza gharama kubwa mno katika maisha, kwani pesa nyingi huitajika katika kujitibu. 

Pia sisi kama watu na taifa linaloendelea kukua kiuchumi, kimazingira, kijamii na kitekenologia basi si vyema tukabaki nyuma katika suala zima la usafi. Ni wajibu wetu na wa kila mwananchi kutunza mazingira yake. Hili pia linaweza kusaidia kupunguza pesa nyingi zinazopotea katika kutunza mazingira ambayo kila mmoja wetu anawajibu huo. 

Ni matumaini yangu kuwa kwa waraka huu mfupi, kila mmoja wetu atakayepata nafasi ya kuupitia, atafahamu nini umuhimu wa usafi na kwanini nimekuwa nikiunga mkono harakati za wana-Moshi katika kutunza na kudumisha usafi wa manispaa yao. 

Mtanzania Badilika Sasa!!!  

Friday, October 26, 2012

EID MUBARAK


MMILIKI WA BLOG HII (Maxmillian Kattikiro) ANAPENDA KUWATAKIA WATANZANIA WOTE NA WADAU WOTE WA BLOG HII "EID MUBARAK" NJEMA NA FURAHA KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU HII.

Thursday, October 25, 2012

UGANDA: MADAI YA UN DHIDI YETU SIO KWELI



Uganda inatishia kujiondoa katika mazungumzo ya kuleta amani katika nchi kadhaa barani Afrika.

Tisho hilo linafuatIa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyokashifu Uganda kwa madai ya kuunga mkono makundi ya waasi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waziri wa serikali , Asuman Kiyingi, alisema kuwa dhana kuwa Uganda inaunga mkono waasi wa M23 katika DRC wakati ikiwa mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani ni njama ya kuidhalilisha na kuiharibia sifa nchi hiyo.

Aliongeza kuwa , ikiwa madai hayo hayataondolewa dhidi yake pamoja na juhudi za nchi hiyo kukosa kutambulika, serikali itaondoa wapatanishi wake kwenye mazungumzo ya amani.

Amesema pia vikosi vya nchi hiyo vilivyo nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, pia vitaondolewa.

Vikosi hivyo vinaungwa mkono na Umoja wa Mataifa hatika harakati zao dhidi ya waasi na wanamgambo.

UMOJA WA MATAIFA WAITAKA TANZANIA KULINDA MISITU


Climate Change Advisor at United Nations Development Programme, Dr Amani Ngusaru

Mshauri mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa katika Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Amani Ngusaru aliwataka Watanzania wanaoishi karibu na Msitu wa Pugu kukumbatia mfumo endelevu wa maisha. 

"Mnazo changamoto nyingi zikiwemo kuongezeka kwa uchafuzi wa hali ya hewa, na katika suala hili, maendeleo endelevu ni muhimu na kila mtu analazimika kuyalinda mazingira," Ngusaru alisema, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Tanzania.

Msitu wa Pugu ni moja ya mfumo wa ikolojia mkongwe kabisa ulimwenguni, ambao ni makazi ya aina 80 za ndege na maji safi ya Mto Msimbazi ambayo yanatoa maji ya kunywa kwa jamii za jirani, alisema, na kuongeza kuwa unahitajika kulindwa kutokana na athari hasi za mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile upungufu wa maji, umalizaji wa mfumo wa ikolojia, upatikanaji duni wa nishati na kuenea kwa jangwa. 

Ngusaru aliwataka Watanzania kuangalia katika matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala na majiko ya kupikia ya kuokoa nishati ili kusaidia juhudi za serikali za kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuboresha shughuli za maendeleo endelevu.

KESI YA MWANGOSI: MTUHUMIWA AFICHWA SURA


Mtuhumiwa Pacficus akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali 

JESHI la Polisi mkoani Iringa, limeendeleza usiri mkubwa wa kumficha mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Ikiwa ni mara ya tatu kwa mtuhumiwa huyo, Pasificus Cleophace Simon (23), kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jana, ulinzi mkali ulitawala eneo hilo, huku waandishi wakipigwa vikumbo wakizuiwa kupiga picha.

Askari wenye sare wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakiwa na virungu, silaha za moto huku wengine wakivalia kiraia, walitanda mahakamani hapo kuhakikisha hakuna mwandishi anampiga picha mtuhumiwa huyo.

Katika patashika hiyo, mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Eliasa Ally, alijikuta akipigwa na askari ambao walikuwa wakimzuia kupiga picha.

Askari aliyempiga mwandishi huyo alitambulika kwa jina moja la Idirisa, na hivyo tukio hilo likazidisha uhasama baina ya jeshi hilo mkoani hapa na waandishi wa habari.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani akiwa amevalia jaketi lenye kofia iliyomfunika kichwa kizima kiasi cha sura yake kutotambulika.

Akiwa mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka ya mtuhumiwa huyo, Lilian Ngilangwa, alimweleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Dyness Lyimo, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Lyimo aliomba kesi hiyo ihairishwe hadi Novemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.

Pasificus alifikishwa mahakamani hapo, akidaiwa kumuua kwa makusudi Mwangosi wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, mnamo Septemba 2, mwaka huu.

MHESHIMIWA RAIS MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, BENJAMIN WILLIAM MKAPA ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NYUMBANI KWA BALOZI WA TANZANIA UBELGIJI MH. DKT. DIODORUS KAMALA TAREHE 21.10.2012...!!!

Mh. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akikaribishwa na Mama Balozi mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Brussels kwa ajili ya chakula cha jioni
 Pichani ni baadhi ya watanzania na maafisa ubalozi waliojitokeza kumpokea Mh. Mkapa
 Mh. Mkapa akisaliana na wadau
  Ukaribisho ukiendelea
 Wakina mama hawkaubaki nyuma
 Mh. Mkapa akikaribishwa
 Baadhi ya watanzania waliojumika na Mh. Mkapa ktaika chakula cha jioni nyumbani kwa Mh. Balozi Kamala
 Rais mstaffu wa Tanzania Mh. Benjami Mkapa akiwa katika picha na Mh. Balozi wa Tanzania Belgium Dr Kamala nyumbani kwake
 Rais mstaafu wa Tanznia Mh. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kikundi cha Upendo cha Ubeligiji na Mh. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Kamala
 Rais mstaafu wa Tanzania Mh. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na familia ya balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr Kamala
 Baadhi ya viongozi wa Jumuyia ya watazania Ubeligiji na Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja na Rais msatafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa pamoja na balozi wa Tanzania Ubelgiji Mh. Dr Kamala