To Chat with me click here
Showing posts with label Elimu. Show all posts
Showing posts with label Elimu. Show all posts

Friday, June 20, 2014

MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO HAYA HAPA!



Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2014 ambao waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013

Wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa kuanzia tarehe 10 Julai 2014 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 30 Julai 2014. 

Aidha, hakutakuwa na mabadiliko ya wanafunzi kubadilishiwa shule walizopangiwa, hivyo wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kama inavyoonekana katika matokeo haya.



MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2014

 






Maxmillian Kattikiro Blog  inapenda kuwapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na sita kwa mwaka 2014. Pia tunapenda kuwatia moyo wale wote ambao hawakuchaguliwa kuwa, wasikate tama, bado wanayo nafasi nzuri ya kurekebisha pale ambapo walitereza, na vilevile watambue kuwa elimu haina mwisho.
 

Tuesday, September 17, 2013

BREAKING NEWS!!!! SEKONDARI YA ILBORU VIPAJI MAALUM YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KWA HOFU YA KUCHOMWA MOTO...

SHULE ya Sekondari ya Ilboru, jijini Arusha imefungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo baada ya kuwepo hofu ya kuchomwa moto.

Uchunguzi wa madai ya shule hiyo kuchomwa moto, unaendelea kufanywa huku ikielezwa kwamba wanafunzi wanne wanahojiwa na polisi wilayani Arumeru wasaidie kubaini ukweli juu ya madai hayo.

Wanafunzi wengine 10 inadaiwa wamepewa barua za kusimamishwa shule kwa siku kadhaa wakihusishwa na suala hilo.

Tangazo la kufunga shule hiyo lilitolewa ghafla leo asubuhi na Mkuu wa Shule, Julius Shila baada ya kushauriana na bodi yake, huku polisi wa kawaida wakifanya doria kudhibiti vurugu zozote ambazo zingeweza kutokea.

Ingawa Mkuu wa Shule, Shila hakutaka kuzungumzia suala hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Mkoa, Sifael Mollel, alisema uchunguzi wa madai hayo unaendelea katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wamepewa likizo.

Alisema kuwepo kwa hofu hiyo na wasiwasi wa kuzuka vurugu ndiko kulikosababisha shule ifungwe kwa muda licha ya kwamba walikuwa hawajamaliza mitihani.

“Uongozi umeamua wanafunzi warudishwe nyumbani kutokana na hofu ya kuchomwa moto shule, wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani kabla ya kuanza likizo fupi lakini uwepo tishio hilo na kuzuka kwa vurugu, ilionekana ni vema ikafungwa,” amesema.

Alisema kwa kawaida likizo fupi ni ya siku 10 lakini kwa tukio hili wanafunzi hao wamepewa maelekezo ya kwenda kuonana na wakuu wa wilaya zao kwa udahili kabla ya kurejea tena shuleni.

Akizungumzia vitisho vya moto, alisema wanafunzi hao waliwasilisha barua ofisini kwake wakitoa madai kuwa baadhi ya walimu walikuwa wanataka kuchoma moto shule hiyo.

Alisema polisi walienda kufanya uchunguzi Ijumaa ambapo walinusa harufu ya petroli iliyokuwa imemwagwa jirani na bweni.

Hata hivyo Kaimu Ofisa Elimu huyo hakutawataja wanafunzi ambao wanahojiwa na polisi wala wanafunzi 10 ambao wamesimamishwa kwa siku 21.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas, alikiri polisi kuwepo shuleni hapo wakati tangazo la kufungwa shule likitolewa akasema hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya kuimarisha usalama.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, wanafunzi wote watatakiwa kurejea shuleni hapo baada ya kudahiliwa na wakuu wa wilaya zao.

Tuesday, June 4, 2013

KAWAMBWA KITANZINI LEO, BAJETI YAKE HATARINI KUPITISHWA



Dodoma,Tanzania

Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa
WAKATI Watanzania wakijiandaa kufuatilia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya  Mafunzo ya Ufundi leo Waziri wa Wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa anatarajia kukutana na upinzani mkali, kutoka kwa wabunge wa pande zote mbili yaani Upande wa Upinzani na Wapunge wa CCM.

Habari zilizonaswa na Vyanzo vyetu vya habari zinadai kwamba, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM mjini Dodoma zinadai kwamba, Wabunge hao wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo ajiuzuru ili kukisafisha Chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli kwa Wanafunzi mwaka huu.

"Hotuba ya Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama Kawambwa hata jiuzuru, hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ndiyo inayochangia kuharibu Chama"kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa majina yake na kuongeza:

"Huu mpango unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshma ya Chama, lakizima tuanzie ndani kuwajibishana wenywe kabla ya wapinzani kuanza, kwani tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi na hatimaye watazidi kuichukia Serikali". Wakati Waziri Dk Kawambwa akiandaliwa mazingira ya kung'olewa, Necta inatarajia kutangaza matokeo yaliyoongeza kiwango  cha  ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57, wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.