To Chat with me click here
Showing posts with label Ufisadi. Show all posts
Showing posts with label Ufisadi. Show all posts

Sunday, June 1, 2014

KASHFA SABA NZITO NCHINI!




Dar es Salaam.
Serikali imepoteza zaidi ya Sh362.9 bilioni kutokana na baadhi ya kashfa kubwa za ufisadi na operesheni mbalimbali zilizoligharimu taifa tangu uhuru.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini taifa kukumbwa na kashfa mbalimbali za upotevu wa fedha au kuanzisha mipango ambayo utekelezaji wake ulisababisha maumivu kwa wananchi na hakuna awamu ya uongozi wa Serikali iliyokwepa hali hiyo.

Kuanzia awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere aliyeiongoza nchi toka mwaka 1961 ilipopata uhuru hadi 1986, Rais Ali Hassan Mwinyi (1986-1995), Rais Benjamin Mkapa (1995-2005) na Rais Jakaya Kikwete (2005-hadi sasa), kumeibuka kashfa mbalimbali, saba zikiwa kubwa na kulitikisa taifa.

Kashfa na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa ni pamoja na Operesheni Uhujumu Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS) na Kashfa ya Rada.

Nyingine ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na ile ya uchotaji mabilioni katika akaunti ya Escrow.

Operesheni Uhujumu Uchumi
Mwaka 1984 Serikali ilianzisha Operesheni Uhujumu Uchumi, iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Sokoine ili kutaifisha mali ambazo baadhi ya watu walidaiwa kujipatia kwa njia isiyo halali.

Operesheni hiyo ilishuhudia baadhi ya watuhumiwa wakimwaga fedha mitaani na majalalani, huku wengine wakitupa mali kuhofia kutiwa kwenye mkono wa sheria.

Hata hivyo, katika operesheni hiyo baadhi ya watendaji wa Serikali ambao hawakuwa waaminifu, waliitumia nafasi hiyo vibaya kutaifisha mali za baadhi ya watu, ambao hawakuwa wahujumu uchumi.

Zoezi hilo lilisababisha wananchi kadhaa hasa vijijini kuwekwa ndani na wengine kuachwa maskini baada ya kunyang’anywa mali zao ikiwamo mifugo na mashine za kusaga nafaka, kwa kudaiwa kuwa walizipata kwa njia isiyo halali.

Mfuko wa Commodity Import Support (CIS)
Miaka 24 baadaye yaani mwaka 2008, liliibuka sakata jingine lililokuwa na harufu kubwa ya ufisadi wa mabilioni katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS).

Sakata hilo liliwahusisha baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara maarufu nchini na wizara kadhaa za Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kupitia mfuko huo, vigogo hao walichota zaidi ya Sh200 bilioni kwa kivuli cha uagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi.

Mfuko huo wa CIS, ulianzishwa katika miaka ya 1980, ambapo baadhi ya nchi wafadhili ikiwamo Japan, zililenga kuipatia Tanzania fedha za kigeni za kununulia malighafi, vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo, ujenzi na vingine mbalimbali. Mpango huo ulioanzishwa na Serikali uliendelea hadi mwanzoni mwa miaka 2000, ambapo nchi hizo wahisani ikiwamo Japan, Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Sweden na Denmark zilikuwa zikiipatia Serikali fedha za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.

Wizara zilizotajwa katika orodha ya wadeni wa CIS ni pamoja na iliyokuwa ya Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Kazi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Tanzania Bara, wakati Zanzibar zinatajwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Maji.

Rada
Mwaka 2011 Serikali ilikumbwa na jinamizi la ufisadi kwa mara nyingine. Safari hii uliibuka ufisadi wa mabilioni ya shilingi kupitia ununuzi wa rada kuukuu kutoka Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza. Ununuzi wa rada hiyo unatajwa kutofuata taratibu sahihi, uliligharimu taifa Sh29.5 bilioni, wakati gharama halisi ilikuwa Sh21 bilioni.

Serikali ya Uingereza iliamua kurudisha fedha hizo kama chenji, huku ikisisitiza kuwa watuhumiwa wote wa hapa nchini waliohusika na ununuzi wa rada hiyo mtumba, washitakiwe Tanzania au Uingereza kutokana na kubainika dosari kwenye ununuzi huo.

Wakati Uingereza ikitaka watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani, mtandao wa Wikileaks unaosifika kwa kufichua siri za ndani ya mataifa mbalimbali duniani, ulibaini kuwepo kwa harakati nchini za kutowafikisha mahakamani wahusika wa ufisadi huo.

EPA
Mwaka 2008 iliibuka kashfa nyingine ya wizi wa mabilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ambapo vigogo kadhaa walitumia mbinu chafu kuchota zaidi ya Sh133 bilioni katika akaunti hiyo.

Katika wizi huo ulioitikisa nchi, wahusika walitajwa kutumia vivuli vya siasa katika kupitisha nyaraka bila kufanyiwa uhakiki wa nyaraka hizo.

Friday, May 16, 2014

REVEALED: WHO GOT PAID THE TSH201BN ESCROW CASH!



RE-POSTED NEWS!

The $122 million (Sh201 billion), which was at the escrow account held at Bank of Tanzania (BoT), was transferred to Pan Africa Power Solutions (Tanzania) Ltd (PAP) account between November 28 and December 8, last year (2013).

This revelation comes at a time when Standard Chartered Bank, Hong Kong (SCB – HK), through its lawyers, has given Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) a 30-day ultimatum to re-deposit the money into the account or else face legal consequences.

An escrow account is a financial instrument held by a third party on behalf of other two parties in a transaction. The funds are held by this kind of account until it receives the appropriate written or oral instructions or until obligations have been fulfilled.

Contrary to claims by the ministry of Energy and Minerals that the escrow monies were paid to Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), The Sources have reliably established that the $122 million was actually paid to PAP.

PAP is the company that has acquired IPTL by using the escrow funds in a deal that has been queried by some legal experts, who are wondering how a once liquidated company became the assignee, and assigned its shares to a new investor.

According to details gathered by The Sources, which are also corroborated by official correspondence from the BoT to the Treasury, the agreement to release the escrow billions was signed on October 27, 2013.

In a letter dated December 19, 2013, BoT deputy governor responsible for administration and internal controls, Mr Juma Reli, wrote: “Invoking the provisions of Articles 7.7 of the Agreement, GOT and IPTL executed an agreement for delivery of the escrow funds to IPTL…the agreement for delivery was signed on October 27, 2013, pursuant to which the bank was instructed to release the escrow fund.

In a letter directed to the permanent secretary of the ministry of Finance, Dr Servacius Likwelile, Mr Reli, further writes: “The funds together with un-matured investments in treasury bills were dully transferred to IPTL on November 28, 2013 and December 5, 2013.”

“In view of the foregoing, we hereby request you to order the closure of the escrow account…simultaneously we wish to kindly inform you that with effect from December 5, 2013 when the last transfer was effected, the Bank has been duly discharged from its role and obligations as an escrow agent with respect to Power Purchase Agreement between IPTL and Tanesco.”

Though the BoT says it transferred the escrow funds to IPTL, the affidavit sworn by James Rugemalira, managing director of VIP Engineering and Marketing Ltd, served at the High Court on January 8, year 2014, state that the money was paid to PAP.

VIP Engineering and Marketing Ltd was a Tanzania company that owned 30 per cent shares in IPTL until it allegedly sold its stakes to PAP at the cost of $65 million (Sh129 billion)—the income he described last week as “just few cents for tobacco.”

Just a day after the BoT letter, the government chief legal counsel, Attorney General Justice Frederick Werema, wrote to Hunton and Williams LLP, a US law firm representing Tanesco, stating: “This letter (BoT letter) is instructive…it may be helpful to any measures that you may wish to pursue on behalf of your client.”
Ministry’s contradictory versionIn another development, the ministry of Energy and Minerals issued two conflicting communications last week, in a bid to defend what transpired between IPTL, Tanesco and Pan Africa Power Solutions (PAP).

UFISADI BIL. 200 BOT: VIGOGO WAUNDA ZENGWE KUKWEPA!

Mengi, Mkono wazushiwa kumchafua Muhongo; Dk. Slaa asema ni baada ya Bunge kugeuka kichaka


MKAKATI wa kuwanasua vigogo wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa nzito ya ufisadi wa dola za Marekani milioni 122 (sawa na sh bilioni 200) katika akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (Escrow) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umeanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Waraka ambao umeandikwa na mtu anayejitambulisha kama mhasibu wa Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), unawataja Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, kuwa ndio wanaeneza tuhuma hizo kwa lengo la kuwachafua Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi.

Huu ni mnyukano unaotokana na tuhuma za Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), kuhusu vigogo sita wa serikali wakiwemo mawaziri kadhaa aliodai wamehusika na ufisadi wa fedha hizo zilizokuwa zimewekwa katika akaunti ya Escrow.

Kafulila aliwataja Waziri Muhongo na Katibu Mkuu wake, Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Alisema kuwa ufisadi huo ni lazima mbivu na mbichi zifahamike, na kwamba haungi mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hili kwa kuwa linagusa mamlaka kubwa katika dola, badala yake iundwe Kamati Teule ya Bunge.

Katika kile kinachoonekana kama mkakati wa kuhamisha hoja ya msingi, jana ulisambazwa waraka kwenye mitandao ya kijamii ukiwa umeandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu ukisomeka “Sakata la IPTL mchezo wa wanasheria na wafanyabiashara”.

Mwandishi wa waraka huo anasema; “Mimi ni Mtanzania mwajiriwa wa Tanesco, kwa muda mrefu nimekuwa nikilifuatilia suala la IPTL linavyokwenda na linavyojadiliwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo bungeni.

“Naomba niwaeleze kwamba suala hili naona wengi hawalielewi, bali wanaongea kwa jazba na ushabiki kwa kitu wasichokijua kabisa na huenda labda wanatumiwa na watu wenye maslahi na Shirika letu la Tanesco,” alisema.
Alifafanua kuwa suala la Tanesco, IPTL na akaunti ya Escrow ni la kisheria zaidi na si suala la kisiasa, na kwamba tusipokuwa makini tutajikuta tunaingia katika masuala yasiyokuwa ya msingi na tukajuta baadaye.

“Mimi kama Mhasibu wa Tanesco, nakumbuka Escrow ilifunguliwa tarehe 5 July, 2006 wakati mkataba wa IPTL na Tanesco uliingiwa mwaka 1995 na lengo lake lilikuwa ni kuweka fedha za Capacity charges ambazo zilikuwa na mgogoro kutokana na Tanesco kupinga gharama hizo, lakini wakati huo huo walikuwa wakitumia umeme wa IPTL.

Thursday, May 2, 2013

TUHUMA: VIGOGO, WAKALIA MABILIONI YA CIS



Mhe. Kimbisa
Dar es Salaam. Baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na wizara kadhaa za Serikali za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wameendelea kukalia mabilioni ya shilingi waliyokopa kupitia uliokuwa Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya Nchi (Commodity Import Support - CIS).

Taarifa ambazo zimetufikia zinasema kiasi cha fedha ambacho bado hakijarejeshwa na wakopaji hao ni Sh216 bilioni ambazo kama zingepatikana, zingetosha kugharimia madawati milioni 2.7 kwa gharama ya Sh80,000 kila moja yenye uwezo wa kutosheleza wanafunzi milioni 8.1.

CIS ni mpango ulioanzishwa na Serikali miaka ya 1980 na kuendelea hadi mwanzoni mwa miaka 2000, ambao nchi wahisani zikiongozwa na Japan zilikuwa zikiipatia Serikali fedha za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.

Nchi nyingine zilizochangia fedha hizo ni Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Sweden na Denmark na madeni yaliyotokana na fedha hizo ni sehemu ya deni la taifa ambalo linagharimiwa na fedha za walipakodi wa sasa.

Hata hivyo, taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mpango huo ni kama ulihujumiwa na baadhi ya waliochota fedha hizo kwani walizitumia kinyume cha makusudio na sasa ni kama Serikali imeshindwa kuzirejesha licha ya kumwajiri mkusanyaji kwa mwaka mzima.

Fedha hizo zilitakiwa kutumika kununulia malighafi, vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo na ujenzi, wakati huo hali ya uchumi hususan ya upatikanaji wa fedha za kigeni ilikuwa mbaya, hivyo mpango huu ulikuwa usaidie kuinusuru hali hiyo.

Mwanzoni mwa 2011, Serikali iliingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya udalali ya Msolopa Investiment Limited ambayo kwa mujibu wa taarifa za uhakika, mkataba wake ulimalizika Januari mwaka jana bila kutimiza lengo la kurejesha mabilioni hayo.

Mkataba huo ulifikia ukomo huku Msolopa ikiwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh5 bilioni, sawa na asilimia 2.31 tu ya Sh216 bilioni ambazo bado zinadaiwa mikononi mwa wakopaji. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msolopa, Ibrahim Msolopa alikataa kuzungumzia suala hilo akisema hana mamlaka...
“Mkataba wangu na Serikali juu ya suala hilo ulishafikia ukomo, nimeshakabidhi kila kitu kinachohusu CIS kwa Serikali kwa hiyo kama mnahitaji taarifa yoyote nendeni serikalini.”

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema halifahamu suala la watu kudaiwa fedha za CIS... “Ninahitaji muda wa kulifuatilia suala hili na kufahamu undani wake.”

Vigogo wanaodaiwa
Uchunguzi umebaini kuwa fedha hizo zimekaliwa na wafanyabiashara na wanasiasa kupitia kampuni zao wakiwamo wabunge wa CCM, Abbas Mtemvu (Temeke) na Henry Shekifu (Lushoto), Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Ramadhan Madabida (Dar es Salaam) na Adam Kimbisa (Dodoma).

Kampuni ya Shamshi & Sons ya Shekifu ilikopa Yen za Kijapani 12,778,082.81 (sawa na Sh.207 milioni) kwa kuzingatia viwango vya sasa vya kubadilisha fedha ambavyo ni wastani wa Sh16.20 dhidi ya Yen moja.

Kampuni ya Cargo Plan International, ambayo mmiliki wake ni Kimbisa ilikopa Yen 2,882,961.79 (zaidi ya Sh46.7 milioni), wakati Tanzania Pharmaceutical inayomilikiwa na Madabida ilikopa Yen 7,031,983.29 (takriban Sh114 milioni).
Kampuni ya A.M.General Agency inayomilikiwa na Mtemvu ilikopa Yen 20,000,000 (sawa na Sh324 milioni). Taarifa zinaonyesha kuwa madeni hayo hayajalipwa.

Wednesday, December 19, 2012

MAFISADI WALIOFICHA MABILIONI NJE WAANZA KUSAKWA


Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa

Serikali inafanya mawasiliano na nchi zinazotajwa ikiwamo Uswisi kuwa baadhi ya vigogo wake wamehifadhi mabilioni ya Shilingi.

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amesema katika kushughulikia madai hayo, Serikali ya Tanzania imeanza rasmi mchakato wa kubaini maeneo halisi zilikofichwa fedha hizo.

Dk. Mgimwa aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoani Iringa (CCM), Ritha Kabati kupitia mradi wa Decision Foundation.

Katika mahojiano yake na waandishi wa habari, Dk. Mgimwa ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga, alisema  ni ukweli usiopingika kwamba utoroshwaji wa mabilioni hayo ya fedha kwenda nje ya nchi unachangia uchumi wa taifa kudumaa.

Aidha, alisema mtu yeyote aliyehamisha fedha hizo kiharamu na kuwekeza nje ya nchi, atashughulikiwa kuanzia sasa kwa kuwa taratibu na uchunguzi zimeanza.

Waziri Mgimwa alisema lengo la uchunguzi huo ni kutambua fedha hizo zilipelekwa ughaibuni kwa makusudi gani, ni Shilingi ngapi pamoja na kuhakikisha serikali inawatambua kwa majina yao.

“Tumeanza kufanya mawasiliano na nchi ambazo zinatajwa kuhusika katika uhifadhi wa mabilioni hayo kwa hiyo serikali imeanza uchunguzi ikitaka kufahamu kiwango cha fedha kilichotoroshwa ili kutambua serikali imepata hasara kiasi gani na hatimaye wahusika wa tuhuma hizo kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

Aliongeza: “Yeyote aliyewekeza fedha hizo nje ya nchi atashughulikiwa, kwa sababu hali hii inasababisha matatizo kwa taifa na wananchi kutokana na kuhamisha fedha kiharamu."

Sunday, December 16, 2012

LAZARO NYALANDU, ADAIWA KUMILIKI KAMPUNI YA KITALII, MWENYEWE AJITETEA WAZIRI KAGASHEKI ADUWAA

Naibi Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyarandu
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani) anadaiwa kumiliki kampuni inayojishughulisha na masuala ya utalii kitendo ambacho kinamwingiza kwenye mgongano wa kimasilahi.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyalandu anamiliki Kampuni ya Nitoke Safaris Ltd jambo ambalo limeelezwa kuwa ni kinyume na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa kwa kuwa yeye ni msimamizi wa sekta hiyo.

Taarifa kutoka kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (Brela), zinaonyesha kuwa wamiliki wa Kampuni hiyo ni L.S.Nyalandu na Faraja G. Nyalandu, huku kila mmoja akimiliki asilimia 30 ya hisa.

Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000.

Ofisi za kampuni hiyo ziko PPF Complex Suit, namba 24 Barabara ya Mzingo, Arusha na magari ya kampuni hiyo yamekuwa yakibeba watalii mkoani Arusha.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana akiwa Mwanza, Waziri Nyalandu alikiri kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo lakini akasema tayari alishajitoa.

Katika kujenga hoja ya utetezi wake, Nyalandu alisema kama ambavyo haipendezi yeye kumiliki kampuni ya utalii akiwa waziri wa wizara hiyo, haitapendeza pia waziri wa habari kumiliki gazeti.

“Huwezi kuwa Waziri wa Utalii na ukafanya biashara ya utalii huko katika kampuni hiyo mie nilishatoka kitambo,” alisema bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, kumbukumbu za Brela zinaonyesha kuwa waziri huyo bado ni mmoja wa wanahisa ingawa haijafahamika kama ni tatizo la Brela kutorekebisha kumbukumbu za jalada lake baada ya kujitoa au la.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki alipoulizwa na gazeti hili jana alionyesha kushtushwa na taarifa hizo na kusema hajui kama Naibu wake anamiliki kampuni ya utalii.

“Siwezi ku comment (kutoa maoni), chochote juu ya jambo hilo kwa sababu sijui kama ana kampuni ya utalii na pili, ndiyo kwanza nasikia hizo taarifa kutoka kwako (mwandishi),” alisema Kagasheki.

Taarifa zilizowakariri baadhi ya mawakala wa utalii mikoa ya Kilimanjaro na Arusha zilidai kuwa Nyalandu ni mmoja wa washindani katika biashara hasa ya kwenda mbuga za wanyama.

Haijafahamika kama Nyalandu aliwahi kutangaza kuwa na masilahi na kampuni hiyo au kama aliwahi kuiorodhesha kama moja ya mali anazomiliki kama Sheria ya Maadili ya Viongozi inavyotaka.

“Siyo tatizo kiongozi kumiliki kampuni, lakini unatakiwa ku-declare interest (kutangaza masilahi) lakini kwa Nyalandu ni tofauti kidogo kwa sababu sasa yuko kwenye sekta hiyo,” alidokeza wakili mmoja.

Wakili huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema hata kama Nyalandu atakuwa haipi upendeleo kampuni hiyo, lakini kwa akili ya kawaida, ni rahisi binadamu kuhisi kampuni hiyo itakuwa ikipewa upendeleo wa aina fulani.
Hata hivyo, Wakili mwingine, Albert Msando wa Arusha, alisema kwa dhana nzima ya utawala bora, Waziri wa Maliasili na Utalii au Naibu wake au watendaji wa Tanapa hawapaswi kumiliki kampuni ya utalii.

“Kwa waziri ku-declare interest (kutangaza masilahi), haitoshi kwa sababu kwanza ndiyo itachochea zaidi watu kufanya biashara na kampuni yako hata kama hauko kwenye utendaji wa kila siku,” alisema.

Friday, November 9, 2012

UFISADI WA KUTISHA UZINDUZI JIJI LA ARUSHA


Rais Kikwete akizundua Jiji la Arusha.

UZINDUZI wa Jiji la Arusha uliofanyika wiki Ijumaa iliyopita (Oktoba 2,2012) umekomba hazina ya Jiji hilo kwa zaidi Sh milioni 100 kutumika kama gharama za sherehe hizo huku malipo mengi yakiwa wamejaa utata.

Jiji hilo lilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid na kuhudhuirwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, kimataifa na wananchi wa Arusha.

Hata hivyo, pamoja na sherehe hizo kufana, tayari kuna taarifa za tuhuma kuwa sherehe hizo ziligubikwa na matumizi makubwa ya fedha za Halmashauri ya Jiji hilo, huku matumizi mengi yakionekana kutokuwa na lazima.

Katika mchanganuo wa awali ambao Raia Mwema imefanikiwa kuuona kama dokezo kwenda kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Omar Mkombole kutoka kwa Mweka Hazina wa Jiji, K.A.Mpakata, Mhazini huyo aliomba kiasi cha Sh milioni 114,149,500 ili kufanikisha sherehe hizo.

Dokezo hilo lenye kumbukumbu namba MD/S.40/7.VOL 111 lililoandikwa Oktoba 30, lilikuwa na kichwa cha habari: “Yah. Gharama za uzinduzi wa Jiji ambazo zimewasilishwa kwa ajili ya malipo mpaka leo tarehe 30/10/2012,” likieleza kwamba katika kikao cha Kamati ya Fedha kilichofanyika Oktoba 23, mwaka huu, kiasi cha Sh 66,000,000 ziliombwa kwa ajili ya shughuli za uzinduzi wa Jiji, na kwamba makizio ya gharama hizo yalikuwa kabla ya ujio wa Rais Jakaya Kikwete.

“Lengo la kuandika barua hii ni kuonyesha hali halisi ya gharama tofauti na makisio yaliyopitishwa na kikao cha Kamati ya Fedha cha tarehe 23/10/2012,” lilisomeka dokezo hilo.

Habari zilizofikia Raia Mwema baada ya sherehe hizo za uzinduzi wa Jiji la Arusha, zinabanisha kwamba kiasi cha fedha hizo Sh milioni 100 zilizombwa katika dokezo hilo la Mweka Hazina, kilipunguzwa hadi kufikia zaidi ya milioni 95, kabla ya Kamati ya Fedha kukutana tena, huku sehemu kubwa ya fedha hizo ikiwa tayari matumizi yake yamefanywa na Mweka Hazina huyo pamoja na watumishi wengine wa Idara ya Fedha.

Kwa mujibu wa mchanganuo uliopo, fedha ambazo malipo yake yamezua utata katika dokezo hilo, yamehusu malipo kwa kikundi cha wasanii maarufu cha Orijino Komedi kutoka jijini Dar es Salaam, ambacho kinadaiwa kulipwa Sh milioni 12.0.

Malipo ya kiasi hicho cha fedha yalizua utata mkubwa hata katika kikao cha Baraza la Madiwani ambapo awali ilidaiwa kuwa wasanii hao walikubalina na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, kulipwa kiasi cha Sh milioni 5.0 kwa shughuli ya kutoa burudani katika sherehe hizo.

“Katika hali ya kushangaza, Mweka Hazina alilipa milioni saba zaidi tofauti na makubaliano ya awali na mkuu wa wilaya, kwamba wasanii hao wangelipwa Shilingi milioni tano tu,” kinaeleza chanzo chetu cha habari hizi.

Monday, October 1, 2012

KASHFA NYINGINE YAIBUKA TANESCO


KASHFA mpya imeibuka ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya kubainika kuwa vikombe vya kufungia nyaya za umeme vyenye thamani ya mamilioni ya fedha vimetelekezwa kutokana na baadhi ya vigogo wa shirika hilo kushindwa kunufaika na mradi huo.

Habari kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa vigogo hao wanadaiwa kuvikataa vikombe hivyo kwa maelezo kuwa ni vibovu, baada ya mzabuni kushindwa kuwaona vigogo hao. Wakati vigogo hao wakivikataa vikombe hivyo kwa madai kuwa ni vibovu, taarifa zinaeleza kuwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamethibitisha kuwa vikombe hivyo ni vizuri na havina matatizo yoyote. Hatua ya Tanesco kupeleka vikombe hivyo kuthibitishwa na wataalamu wa Chuo Kikuu, Kitengo cha Uhandisi ilitokana na mvutano uliokuwapo baada ya vigogo walioshindwa kunufaika na mradi huo kutoa maelezo kuwa vikombe hivyo havina viwango bora. 

Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa licha ya vigogo hao kuvikataa vikombe hivyo zaidi ya 40,000 vyenye thamani ya Sh900 milioni kwa madai kuwa vibovu, tayari shirika hilo limekuwa likivitumia katika nguzo zake zenye umeme mkubwa kwa miaka mingi. Mvutano wa viongozi hao ndani ya shirika hilo, umesababisha mradi wa kukarabati njia za umeme mkubwa bila ya kuzima umeme kwa kuondoa vikombe vilivyochakaa uliokuwa ukifanyika katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kusimamishwa mapema mwaka huu. 

Baadhi ya wataalamu wa Tanesco wanaeleza kuwa vikombe hivyo kama vitatumika vina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya kufunga vikombe vipya katika njia ya umeme mkubwa wa kutoka kwenye mtambo wa kuzalishia umeme wa Kidatu mkoani Morogoro hadi Ubungo jijini Dar es Salaam. Pia, kumalizia ukarabati wa njia ya umeme ya Arusha hadi Moshi mkoani Kilimanjaro iliyositishwa. 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Tanesco kinaeleza kuwa vikombe vilivyopo katika njia ya umeme ya Kidatu hadi Ubungo havijabadilishwa kwa miaka mingi hali ambayo inafanya umeme kupotea njiani kwa asilimia nyingi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Felschami Mramba alisema kuwa mikataba ndani ya shirika hilo ni mingi na kusisitiza kuwa hawezi kulijibu suala hilo mpaka atakapowasiliana na kitengo cha ununuzi cha shirika hilo. 

“Kwa sasa sina maelezo ya kina ya mikataba, hasa kuhusu suala hilo unaloniuliza, lakini mpaka wiki ijayo nitakuwa nimefuatilia na kupata jibu sahihi,” alisema Mramba. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulika Nishati, George Simbachawene alisema suala hilo halijafika kwake.

 Simbachawene alisisitiza: “Mambo yanayofika katika ofisi yangu huwa kama malalamiko yanayoletwa na watu kutoka Tanesco na sehemu nyingine. Nikiyapata naanza kufuatilia ili kujua nini kinaendelea.” Alisema kuwa Tanesco ni shirika linalojitegemea katika utendaji wake wa kazi na ndiyo maana lina bodi yake, ambayo hukaa na kupanga mambo mbalimbali ya kufanya.

 “Wakati mwingine wizara inaingilia utendaji wa Tanesco kama tunaona kuna mambo hayaendi sawa, ila hili la ununuzi kwa kweli sijui kwa sababu halijafika ofisini kwangu kama lalamiko,” alisema Simbachawene na kushauri kuwa atafutwe Mramba. Hoja ya kuvikataa vikombe hivyo ambayo imekuwa ikitolewa na baadhi ya vigogo hao wa Tanesco ni kwamba vikombe hivyo ni vizito na nguzo haziwezi kuvibeba, vibovu na kwamba havifai katika ule utaratibu wa kufanya matengenezo bila kuzima umeme. Tanesco imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali zikiwamo matumizi mabaya ya fedha za shirika kwa baadhi ya maofisa kutumia zabuni kujinufaisha. Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi William Mhando alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo.

 Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ilieleza kuwa Mhando alisimamishwa kazi pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. 

 Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi wa Ununuzi, Haruni Mattambo. Matatizo mengine ambayo yanadaiwa kuikumba Tanesco ni pamoja na uchakavu wa mitambo ya Tanesco, hujuma za miundombinu na kuingiwa kwa mikataba mibovu

Friday, August 24, 2012

MRAMBA AWANG’ANG’ANIA MKAPA, BALALI


ADAI ASINGEWEZA KUKATAA MAAGIZO YAO

Waziri wa zamani Fedha, Basil Mramba (Kushoto), Waziri wa zamani wa Nishati, Daniel Yona (Katikati) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, wakisubiri kuendelea kwa kesi yao ambapo wote wanatuhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh11.7 Bilioni wakati wa uongozi wao.

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha Basil Mramba, jana aliendelea kumkandamiza aliyekuwa bosi wake na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimhusisha moja kwa moja na kutolewa kwa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers.

Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba.

Alidai kuwa kifungu cha 4.3.1  kilichopo kwenye  mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote  yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi. 

Thursday, August 23, 2012

MRAMBA: NILISAMEHE KODI KWA AMRI YA RAIS MKAPA

CHENGE, CHEYO KUMTOLEA USHAHIDI

 
Basil Mramba (71), Waziri mwandamizi aliyetumikia awamu nne zote za nchi hii katika wizara mbalimbali, jana alianza kujitetea dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kumtaja Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kuwa ndiye aliyemuagiza kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart.

Katika kesi hiyo anayodaiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7, kwa misamaha ya kodi, pia alidai kuwa Mkapa alimuagiza kuhakikisha gharama za kuilipa Kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation, zinatoka ndani ya serikali au Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mramba wakati huo akiwa Waziri wa Fedha, alidai kuwa Mkapa alitoa amri ya kufanya mchakato wa kuileta nchini kampuni hiyo kwa aliyekuwa Gavana wa BoT wakati huo, marehemu Daud Bilali, baada ya kushinda zabuni.

Mramba ambaye ni mshitakiwa wa kwanza kati ya washitakiwa watatu, alitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam huku akiongozwa na mawakili wa utetezi, Herbert Nyange akisaidiana na Peter Swai mbele ya jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Jaji John Utamwa na Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu.

Tuesday, August 21, 2012

SITTA: MSIISUBIRI SERIKALI KUTAJA WALIOFICHA MABILIONI

AWASHANGAA WANAOIPA MUDA HUKU WAKIWAFAHAMU WAHUSIKA, ASEMA HAIWEZEKANI MWANASIASA KATIKA NCHI MASKINI AWE BILIONEA, ATAKA WAKAMATWE WAFIKISHWE MAHAKAMANI

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewataka wanaotangaza kuwafahamu vigogo walioficha mabilioni ya fedha nje ya nchi kuwataja mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao badala ya kuisubiri Serikali kufanya hivyo.Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), imekuja wakati baadhi ya wanasiasa, wakiwamo wabunge kutishia kuwataja watu hao, lakini wakisisitiza kuwa ni pale tu Serikali itakaposhindwa kufanya hivyo.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha la Global Financial Integrity, unaonyesha kuwa tatizo la utoroshaji wa fedha nchini limekuwapo katika awamu zote za Serikali zilizoiongoza Tanzania, lakini Awamu hii ya Nne imetia fora.

Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 1970 hadi 2009, unaonyesha kuwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).

Friday, August 17, 2012

WABUNGE CCM WAHAHA KUJIKOSHA NA UFISADI


WAMWOMBA PINDA AMSIHI SPIKA AWASAFISHE, WASEMA TUHUMA ZINAWAFANYA WASHINDWE KUSHIRIKI SENSA
Kamati inayo ongozwa na Rtd. Brig. Gen. Hassani Ngwilizi mbunge wa Jimbo la Mlalo, wakati wakizungumza na waandishi wa Habari.

TUHUMA za rushwa dhidi ya wabunge juzi zilitawala kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliombwa kuingilia kati ili ‘kuwasafisha’ wenye tuhuma hizo mbele ya jamii. Kikao hicho kiliitishwa pamoja na mambo mengine, kuzungumzia nafasi ya wabunge wa CCM katika kuhamasisha umma kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu na utoaji wa maoni kwa Tume ya Katiba Mpya.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zimesema pamoja na kwamba haikuwa moja ya agenda za mkutano huo, Mbunge wa Bukene, Seleman Zedi alisimama na kuibua kilio cha wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa. Mbunge huyo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda alimweleza Waziri Mkuu kwamba baadhi ya wabunge, hasa wa iliyokuwa kamati yake, wangekwendaje kuhamasisha Sensa majimboni wakati wamechafuka kwa tuhuma za rushwa?

VIGOGO WALIOFICHA FEDHA NJE WABANWA


TAKUKURU YASEMA IMEANZA KUWACHUNGUZA


SIKU moja baada ya Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto, kutishia kuwataja vigogo wa serikali walioficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za nje ya nchi, ikiwa serikali haitawataja, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeibuka na kudai kuwa inazifanyia kazi tuhuma hizo.

Zitto alisema kuwa wamepata taarifa kuwa mmoja  wa viongozi wa juu nchini na baadhi ya mawaziri wa serikali za awamu zilizopita ni miongoni mwa  wamiliki wa fedha hizo zipatazo sh bilioni 314.5.

Alisema sehemu kubwa ya fedha hizo zililipwa na kampuni za utafutaji wa mafuta  na gesi katika pwani ya Mkoa wa Mtwara, zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006, hivyo akaitaka serikali iwataje wahusika na kuwachukulia hatua, vinginevyo atawataja kwa majina.

Tuesday, July 31, 2012

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAMJIBU LISSU


 *Yadai orodha ya Lissu inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge *Anataka kuwaokoa wa Chadema katika sakata hilo.
*Yasema tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe suala la kisiasa Nape akizungumza na waandishi wa habari leo DAR ES SALAAM, TANZANIA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinalaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wana siasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;
"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".

Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.
"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.
"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.

Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.