REST IN PEACE KAMANDA DAUDI MWANGOSI
Daudi Mwangosi, mwanhabari aliyekatizwa maisha na polisi huko Iringa - Jana.
Hapa Polisi wakwataka wafuasi na wanachama wa CHADEMA kutawanyika toka eneo la ofisi za chadema huko Nyororo, Mufindi - Iringa.
Mwili wa Mwanahabari Daudi Mwangosi ukiwa chini.
Daudi Mwangosi kulia anayepiga picha, ilikuwa ni dakika 20 tu kabla mauti kumkuta.
Maxmillian Kattikiro Blog, inaungana na watanzania wote kutoa pole za dhati kwa familia ya Marehemu, Daudi Mwangosi, Kituo cha habari cha Channel Ten, Wanahabari wote kwa ujumla na wote ambao wameguswa na msiba huu.
"Sisi tunatambua mchango wa Mwandosi katika kuhabarisha na kuelimisha jamii yetu, hivyo tunaamini wazi kabisa kwamba Channel Ten wamepata pigo na pengo kubwa sana katika tansinia hiyo ya habari kwa kuondokewa na mpendwa Mwangosi.
Hali kadharika wananchi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla bila kusahau wanahabari wote, tunapaswa kukiri kuwa kuuwawa kwa Daudi Mwangosi kutaacha si simanzi tu mioyoni mwetu bali pengo ambalo halitazibika kamwe, katika nyanja hiyo ya habari".
Hivyo, Maxmillian Kattikiro Blog na wadau wengine wote, tunamwombea kamanda Mwangosi, ili Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake, pia awatie nguvu familia yake hususani katika kipindi hiki kigumu kwao cha kupotelewa na mpendwa wao.
No comments:
Post a Comment