To Chat with me click here

Monday, June 11, 2012

KANISA KATOLIKI LAFANYA MAADHIMISHO YA EKARISTI TAKATIFU


Kwa Wakristo Ekaristi ni sakramenti iliyowekwa na Yesu Kristo wakati wa karamu ya mwisho usiku wa kuamkia Ijumaa Kuu, siku ya mateso na kifo chake.

Jina linatokana na neno la lugha ya Kigiriki (eukharisto: nashukuru) lililotumiwa na Mtume Paulo na Wainjili katika kusimulia karamu hiyo ya mwisho ya Yesu na Mitume wake, na muujiza uliotangulia ambao Yesu alidokeza nia yake ya kushibisha binadamu wote, yaani ule wa kuzidisha mkate na samaki kwa ajili ya umati.

Jina linaonyesha mazingira ya sala ya matukio hayo, ambapo Yesu alimuelekea Mungu akimshukuru kwa vyakula na kinywaji alivyoshika mikononi kabla hajawagawia wanafunzi.Shukrani ilikuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu. “Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, ‘Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu’” (1Kor 11:23-25).

Vipaji vya mkate na divai vilivyoandaliwa kwa adhimisho la ekaristi.

Akizungumza na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia, kama alivyokaririwa na vyanzo vyetu vya habari, Baba Mtakatifu amewakaribisha wote kwa moyo mkunjufu, akiwakumbusha kwamba, Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Mwili na Damu ya Kristo. Maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, kwa namna ya pekee, yanawashirikisha waamini lile Fumbo la "mageuzo uwamo" yanayotokea wakati wa mageuzo ya Mkate na Divai, kuwa ni Mwili na Damu ya Kristo, na hivyo waamini wanampokea Kristo mwenyewe.
Baba Mtakatifu anawakumbusha waamini kwamba, wakati wa maaadhimisho ya Siku kuu ya Mwili na Damu ya Kristo, wanapata fursa ya kumwabudu Yesu katika maumbo ya Mkate na Divai, Sakramenti inayoonesha uwapo wake kati ya waamini wake. Siku kuu ya Mwili na Damu ya Kristo iamshe ari na mwamko mpya katika azma ya kulipenda Fumbo la Ekaristi Takatifu, chemchemi ya neema. 

Kwa Tanzania makanisa yote ya dhehebu hilo, yameadhimisha sikukuu hiyo hapo jana, ambapo hali ilikuwa kama hivi katika kigango cha Mt. Yohane wa Mungu, Parokia ya Yombo Kiwalani, ambapo maandamano hayo yalianzia kanisani hadi makao makuu ya Wakamiliani Tanzania.
 Watoto wa Utatu Mtakatifu wakiwa mbele ya Ekaristi wakati wa maandamano.
Waministranti wakiwa wanafukizia Ubani Ekaristi wakati wa maandamano hayo.
Baadhi ya wanaume wa UWAKA wakiwa katika maandamano pamoja na mwili wa Yesu.
Wanawake "WAWATA" nao hawakuwa nyuma katika kufanya maaadhimisho hayo.
Mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwa wanasubiri Hostia kufika katika sehemu ya maadhimisho katika maeneo ya makao makuu ya Shirika la Wakamiliani - Tanzania.
Padre akitua Hostia mezani baada ya kuifikisha palipo andaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya sikukuu hiyo. Padre akiwaonesha waumini mwili wa Yesu kabla ya kumalizika kwa maadhimisho hayo hapo jana.

No comments:

Post a Comment