HALMASHAURI
Kuu ya CCM (NEC),
imetangaza majina ya wagombea walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
ndani ya chama hicho, huku ikionyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na mchuano
mkali.
Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Mchuano
mkali unaonekana kuwapo kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec Mkoa wa Manyara ambako
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye anachuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.
Mchuano
huo unatarajiwa kuwa mkali katika nafasi ya uenyekiti kwenye baadhi ya mikoa
kutokana na kupitishwa kwa majina ya makada wake maarufu. Mwanza ni miongoni
mwa mikoa hiyo kwani Nec imepitisha jina la Waziri wa zamani wa Maliasili na
Utalii, Anthony Diallo ambaye atachuana na Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo.
Makada
hao watapata ushindani mkali kutoka kwa Zebedayo Athumani, Joseph Yaredi na
Mashimba Hussein Mashimba.
Dar
es Salaam nako kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwani mwenyekiti wa sasa,
John Guninita atachuana na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Makao Makuu ya CCM,
Matson Chizzi na kada mwingine, Ramadhan Madabida. Godfrey Mwalusamba, Harold
Adamson na Paul Laizer wanawania nafasi hiyo mkoani Arusha.
Katika
Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT), ambako Mwenyekiti wa sasa, Sofia
Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anachuana na
Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalumu,
Mayrose Majige.