Kanisa la Kristo Mfalme - Tabata.
Chama cha Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo kuu la Dar-es-Salaam, Jana walifanya maadhimisho ya kutimiza miaka 40 tangu kuasisiwa kwa chama hicho cha kitume ndani ya Jimbo kuu la Dar-es-Salaam kanisa Katoliki. Chama hicho cha kitume kuliasisiwa mnamo mwaka 1972, hivyo mpaka sasa kimetimiza miaka 40 ya utumishi wake katika Kanisa hilo kubwa Duniani na katika Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
Sherehe hizo za kutimiza miaka 40 za WAWATA zilifanyika katika Kanisa la Kristo Mfalme Parokia ya Tabata na kuhudhuliwa na Maaskofu, Mapadre, Masista, Watawa mbalimbali, WAWATA wenyewe na wageni wengine mashuhuli walioalikwa kwenye sherehe hizo.
Maadhimisho hayo yaliambatana na Wanawake hao wa Kikatoliki kufanya maonesho na mauzo ya bidhaa mbalimbali ambazo wamekuwa wakishughulika nazo kama WAWATA, hivyo kutoa fursa kwa watu mbalimbali kujinunulia baadhi ya vitu hivyo.
Sehemu ya Jukwaa Kuu ambalo wageni mashuhuli walikuwa wameketi.
Kikundi cha Kwaya cha WAWATA kikitumbuiza mbele ya Baba Askofu wakati wa sherehe hizo.
Wawata Pichani wakionekana kufuatilia kwa ukaribu juu ya matukio yote katika Sherehe hizo.
Baadhi ya vitu ambavyo wawata wamekuwa wakijishughulisha navyo kama vinavyooneka katika maadhimisho hayo.
nimekupataaa mdau si mchezo fulll information nimeipenda sana ibada ilikuwa nzuri sana
ReplyDeleteHongera Wawata miaka 40 si mchezo umri wa mtu mzima huo
Mdau kama kawaida hapa ni kuhakikisha tunawashirikisha Watanzania habari zote muhimu ili waweze kupata kufahamu juu ya mambo mbalimbali. Tuko pamoja mdau.
ReplyDelete