Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amempongeza Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa (PICHANI) kwa kuteuliwa kwake
kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akichukua nafasi ya
Baba Askofu Yuda Tadei Rwaich aliyemaliza muda wake.
“Nimefarijika
sana na uteuzi wako kushika wadhifa huo muhimu hasa kutokana na imani kubwa
waliyonayo Maaskofu kuhusiana na uwezo wako katika kukiongoza chombo hicho
muhimu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake.
“Ninatambua
na kuthamini mchango mkubwa ambao, kwa muda mrefu sasa, Kanisa Katoliki
limekuwa likuutoa kwa maendeleo ya nchi yetu, hasa katika Nyanja za huduma za
jamii.
Aidha
uhusiano mzurpi kati ya serikali ninayoiongoza na Kanisa Katoliki unaendelea
kunitia moyo, hivyo ninakuhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya nne itaendeleza
nakuimarisha uhusiano huu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla”,
amesema na kusisitiza Rais katika salamu zake za pongezi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar-es-Salaam.
No comments:
Post a Comment