To Chat with me click here

Thursday, July 19, 2012

MH. MNYIKA KUHOJIWA NA KIKOSI MAALUM KUHUSIANA NA MAUAJI YA MWENYEKITI UVCCM SINGIDA.


Sakata la vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi na kupelekea mwenyekitiwa umoja wa vijana (CCM) Yohana Mpinga (30) kuuawa kwa kupigwa kwa fimbo la mawe, limeendelea kuchukua sura mpya zaidi baada ya mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika kuchukuliwa maelezo  na kikosi maalum kutoka Dar-es-salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida, Afisa Habari wa CHADEMA Makao Makuu Tumaini Makene, amesema mbunge Mnyika amefika ofisini kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida akiwa ameitikia wito wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida.
Amesema hata hivyo, Kamanda Sinzumwa amemweleza Mh. Mnyika kuwa anatakiwa kuhojiwa na kikosi maalum kutoka Dar-es-salaam ambacho kwa wakati huo, kilikuwa Ndago kufanya upelelezi wa kitalaam zaidi kuhusina na mauaji ya Yohana.

Hata hivyo, Makene amesema wamepata hofu kwa sababu awali Afisa Sera na Utafiti wa CHADEMA Mwita Waitara, naye aliitwa kwa mtindo unaofanana na huu wa Mh. Mnyika, lakini mwisho wake ikafika mahali akafunguliwa faili na kisha kupelekwa mahakamani.
Katika hatua nyingine Makene amesema CHADEMA inashangazwa na kusikitishwa  na kitendo cha polisi mkoa wa Singida, kushindwa kufanyia kazi majina ya vijana 11 ambao walisababisha vurugu hizo za Ndago.

Ametaja majina ya vijana hao kuwa ni Daniel Sima, Tito Nintwa, Abel John, Martin Manase, Athuman Timbu, James Ernest, Simion Makacha, Anton John, Bakil Ayub, Yohana Makala Mpande na Frank Yesaya.

Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) jijini Dar-es-salaam Mh. John Mnyika (wa kwanza kushoto) akiongozana na mwanasheria wa CHADEMA na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu (wa tatu kushoto) ,wakiingia katika  viwanja vya ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Singida jana jioni (18/7/2012).Mbunge Mnyika aliitwa na jeshi hilo la polisi kuhujiwa juu ya kutio hilo la mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) yaliyotokea julai 14 mwaka huu kwa kusababishwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.Wa kwanza kushoto ni kamanda wa vijana CHADEMA mkoa wa Singida Josephat Isango.anayefuatia mwenye miwani,ni mhadhiri wa chuo kikuu Dar-es-salaam, Dk.Kitila Mkumbo.

 Mbunge jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu akizungumza jambo na kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa.Wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika.

 
Afisa habari wa CHEDEMA makao makuu,Tumaini Makene (wa pili kutoka kushoto
walioketi) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)  juu ya mbunge wa jimbo la Ubungo kuitwa na polisi mkoa kuhojiwa juu ya mauaji ya mwenyikiti wa umoja wa vijana CCM kata ya Ndago.

Jengo la ofisi ya CHADEMA mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment