Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za
pongezi Askofu Protase Rugambwa wa Jimbo Katoliki la Kigoma (pichani), kwa
kuteuliwa kwake na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa XVI
kuwa Katibu Mwambata (Adjunct) wa Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwa ajili
ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, Roma.
“Ninakupongeza kwa
dhati kabisa kwa kuteuliwa kwako katika wadhifa huo mkubwa nikitambua kwamba
uteuzi huo unatokana na imani kubwa aliyo nayo kwako Papa Benedict wa XVI
kutokana na uwezo wako mkubwa kiuongozi na unyenyekevu ulionao kwa watu wako, hivyo nakutakia kila
la kheri na mafanikio makubwa katika kuutumikia wadhifa wako mpya”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za
pongezi.
Aidha Rais Kikwete
amesema anafarijika sana na uteuzi wa Askofu Protase Rugambwa kwa sababu uteuzin huo
umeliletea heshimakubwa Taifa letu nakwa mara nyingine umethibitisha jinsi
viongozi mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wa dini walivyo na imani na uwezo
wa watu wetu katika Nyanja za uongozi.
Askofu Protase Rugambwa
amewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu kumaliza masomo yake ya Teolojia huko
Roma nchini Italia, ambayo hatimaye mwaka 2008 yalimwezesha kuteuliwa na Papa
Benedicti wa XIV kuwa Askofu wa Jimbo la Kigoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar-es-Salaam.
No comments:
Post a Comment