Kattikiro
Internet Café & Stationary (Gongo la
Mboto) ni moja ya ofisi bora zaidi inayotoa huduma ya Intaneti na Steshenari hapo
Gongo la Mboto. Ofisi zetu ni ofisi zenye madhali nzuri kwa wafanyakazi. Ofisi
hii ina kiyoyozi na imetengenezwa (designed) katika hali ya kisasa zaidi ili
kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wetu.
Ofisi
hii itafunguliwa tena hivi karibuni baada ya kuwa imefungwa kwa muda wa miezi
michache iliyopita, hivyo tunahitaji wafanyakazi wawili wa kufanya kazi katika
ofisi hii, wenye sifa na vigezo tunavyovihitaji.
1
Nafasi ya Kazi: Sekretari wa Ofisi
Atawajibika kwa: Mwajiri wake (Director)
Sehemu ya Kazi: Gongo
la Mboto - Mzambarauni
Muda wa Kuanza Kazi: Mara Moja
Kazi na
Majukumu:
·
Kutoa huduma
kwa wateja wetu wote kwa kuuza kulingana na maelekezo
·
Kutunza
kumbukumbu za mauzo kwenye daftali husika
·
Kutoa ripoti
juu ya matatizo yote ya hapo ofisini
·
Kuandaa listi
ya vitu ambavyo vimeisha au kupungua pale ofisini
·
Kukamilisha majukumu
mengine kama itakavyoelekezwa na mwajiri.
Vigezo na
Taaluma:
· Awe mwenye
umri usipungua miaka 18 na si zaidi ya miaka 35
· Awe na elimu
ya Kidato cha nne na kuendelea
· Awe na uwezo
wa kuongea Kiswahili na Kingereza vizuri
· Awe cheti,
stashahada n.k toka chuo
kinachotambulika
· Awe na uzoefu
wa kufanya kazi na Steshenari kwa muda usiopungua mwaka mmoja.
· Ujuzi katika
Adobe Photoshop, Publisher, Coral Draw na Multimedia na ujuzi wa Huduma za Intaneti
ni siza za ziada ambazo zitatoa kipaumbele kwa aliye nazo.
Malipo:
Katikiro Internet Café & stationary huwa
tunawajali sana watu wetu, hivyo tumeandaa malipo mazuri kwa mtu yeyote atakaye
kidhi vigezo vyetu.
Namna ya
Kutuma Maombi:
·
Tuma CV yako
kwa: kattikirointernetcafe@gmail.com
·
Piga simu kwa
namba hizi: +255 614 123160, +255 655 444666, +255 776 444666
Mwisho wa kutuma maombi: ni mwezi mmoja tangu
siku ya tangazo hili (15/08/2012).
No comments:
Post a Comment