Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani
Kinyozi (45), aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa
katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.Pichani ni Rais Kikwete akishiriki
katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo.
Rais
Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu
Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012. PICHA
NA IKULU.
No comments:
Post a Comment