Nimefika
Singida kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa
Iramba kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.
Nimekutana
na RPC, amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa
kuwa kwa sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la
tukio. Nimemuuliza RPC maswali mawili;
1. Wameniita kutoa maelezo kama
mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu
kuwa ni mahojiano ya kawaida.
2. Kwanini mpaka sasa watuhumiwa 12
waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye mwanzo wa mkutano
wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi wakiachia hali
hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM hali ilitulia, Waitara
akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name nikahutubia kwa amani na
kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae mbali na tulipohutubia.
John
John MNYIKA,
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
18
Julai, 2012
No comments:
Post a Comment