Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na
Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,
leo.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi kwenye
Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa,
iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria sherehe za
maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Kutoka (kushoto) Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar,
Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd,
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck
Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe
za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria
maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha
begani.
Ni ishara ya kutoa
heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana
vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika
maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi
wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,
leo.
Huyu ni Mzee CUF, ni maarufu kwa upigaji picha za kuuza 'BANYAA' huyu pia
ni miongoni mwa wapiganaji ambao walipata kupigania haki ya Mtanzania wa leo
enzi hizo, ambaye kwa sasa kazi yake kubwa ni kujishughulisha na uuzaji wa
picha katika shughuli mbalimbali, hapa akihaha kusaka matukio ya kuweka katika
karatasi ya picha zake ambazo baadaye atafanya biashara. Mzee huyu baada ya
kuona siku ya leo ni muhimu hata kwake pia lakini akiweka kazi yake mbele zaidi
ili kujipatika kipato alionelea ni vyema naye pia akakumbukia mavazi yake haya aliyoyavaa
na kutinga nayo eneo la tukio ili kuepuka kusumbuliwa na wahusika aweze kuingia
kirahisi eneo la tukio kama unavyomuona akiwa bize na vazi lake huku akiwa na
begi kubwa la kamera wakati kajikamera alikonako ni kibiriti. Hii yote ni
janja tu ilimradi mkono uende kimiani.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiomba dua kwa
niaba ya waislam wakati wa maadhimisho hayo leo.
Kiongozi wa dini ya kikristo, Mchungaji Kamoyo, akiomba sala kwa niaba ya
wakristo wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,
wakati akiondoka kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo baada ya
kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
No comments:
Post a Comment