*Yadai
orodha ya Lissu inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya
wabunge *Anataka kuwaokoa wa Chadema katika sakata hilo.
*Yasema
tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe suala la kisiasa Nape akizungumza na
waandishi wa habari leo DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimesema kinalaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wana siasa
na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za
rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
Akizungumza
na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya
wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa
baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.
"Mfano
mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na
Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya
wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa
rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;
"Cha
kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua
kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema,
yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".
Nape
alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na
kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.
"Tunamtaka
Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe
nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe
hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.
Alisema
CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa
kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa
nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya
wahujumu uchumi.
"Wakikithibitika
ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa
wengine", alisema Nape.
Nape alisema
CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na
Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na
Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha
kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.
"Tunaamini
uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine
wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili
kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada
zao", alisema Nape.
Alisema,
pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za
nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.
"Tunawaomba
waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo
mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.
No comments:
Post a Comment