CHAMA cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Morogoro kimeendelea kuzoa wanachama kutoka vyama
mbalimbali ambapo juzi jumla ya wanachama wapya 400 walijiunga na chama
hicho.Wanachama hao wapya walijiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya ‘Fire’ mjini hapa. Mwenyekiti wa chama hicho
Manispaa ya Morogoro, Zuberi Kiloko, alisema kati ya wanachama hao 250 ni wapya
huku 150 wakitoka Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Awali, Mwenyekiti wa
Baraza la Wanawake la CHADEMA (Bawacha) Mkoa wa Morogoro, Levina Matambo na
Katibu wa Bawacha, Mecy Naula, waliwashauri wanawake kubadilika na kuunga mkono
juhudi za vyama vya siasa nchini kufanya mabadiliko ya kisiasa kwa kukiondoa chama
kilichopo madarakani na kuingiza chama kipya.
Walisema utawala wa sasa unaongoza nchi kwa mazoea, jambo ambalo linaiingiza nchi kwenye matatizo mbalimbali likiwamo la ugumu wa maisha na huduma duni za kijamii.
No comments:
Post a Comment