Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere. 
Baadhi
  ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa  
kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.
Mwenyekiti
  wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana  
alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya  
kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari  
kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko
  wa ubongo.
 Mwenyekiti  huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege 
aliyosafiri  nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na 
wanaharakati ambao  walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi 
walizani kuwa  angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo 
lakini gari  lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja 
huo. 

 
  
 
No comments:
Post a Comment