Katika
gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka
'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara
baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu
Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema.
Napenda kusema masuala yafuatayo.
Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi. Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimiana na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba
za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa
wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la
kihistoria.
Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.

Kama
mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye
videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na
kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia
yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana
mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.
Suala
la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi
yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza
sana.
Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee
Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio
akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize
yote.
Zitto
Zitto
No comments:
Post a Comment