Mr. & Mrs. Kattikiro Jr |
Kawaida
ifikapo kila 31 December ya kila mwaka, kila mmoja duniani kote hukumbuka au
kusherehekea kumaliza mwaka na kuanza au kuukaribisha mwaka mwingine unaoanza
saa 6 kamili usiku wa siku hiyo. Kwetu sisi kama familia ya Mr. & Mrs.
Kattikiro Junior tumekuwa tukikumbuka juu ya tukio la muhimu sana kwenye maisha
yetu, kwani siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita tuliweza kufunga ndoa
takatifu katika kanisa kuu la Mt. joseph Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
Kwakweli
tumepitia mengi katika mwaka huu mmoja wa maisha ya ndoa, pamekuwa na magumu
mengi, lakini vilevile pamekuwa na neema nyingi mno. Mbali tu na Challenges
nyingi za kimaisha lakini tumekutwa na misukosuko mingi katika maisha yetu ya
kifamilia. Lakini kwa neema za Mungu tumeweza kuendelea kushikamana na kuweza
kujikwamua kutoka katika matatizo na magumu hayo.
Kwa
namna ya pekee kabisa tunapenda kuwashukuru wote ambao wamekuwa msaada mkubwa
kwetu tangu tulipopata wazo la kufunga ndoa na kulikamilisha kulingana na taratibu
za imani yetu hadi kufika leo hii ambapo tunaadhimisha mwaka mmoja wa ndoa.
Tunawashukuru
ndugu zetu wote, familia zetu, majirani na marafiki zetu wote kwa mshikamano,
upendo, na misaada yao ya hali na mali wakati tulipo ihitaji. Tunaomba mzidi
kutusaidia na kutuombea ili tuweze kudumu katika maisha ya ndoa.
Lakini
zaidi ya yote, tunatoa shukurani zetu za pekee kabisa kwa Mwenyezi Mungu, Baba
yetu wa mbinguni, kwakuwa yeye ndiye amekuwa kiongozi wa familia yetu, amejalia
wingi wa neema zako mno, zaidi tunamshukuru kwa kutupatia zawadi ya mtoto wa
kike (Maureen Maxmillian Kattikiro). Kwakweli Jina la Mungu lihimidiwe.
Mwisho
kabisa napenda kuwatakia furaha ya mwaka huu mpya na Baraka tele za Mungu
Mwenyezi ziwe juu yenu nyote, ili sote kwa pamoja tuanze mwaka huu kwa amani na
imani ya kufanikiwa zaidi.
HAPPY
NEW YEAR 2013 !!
MR.
& MRS. KATTIKIRO JR.
31st
DECEMBER 2012
No comments:
Post a Comment