WAKAZI
wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya
wamefariki dunia baada ya kufukiwa wakiwa hai katika kaburi moja na marehemu
wanaodaiwa kumuua, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.
Watu
hao, Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Bibi
Mizinala Nachela ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 50, walizikwa
wakiwa hai pamoja na aliyekuwa mkazi wa kijiji hicho, marehemu Nongwa Hussein.
Kaimu
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili jana
kwa simu kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa tano na sita mchana, muda
mfupi kabla ya maziko ya Hussein.
Kabla
ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, Molela na Nachela kwa nyakati
tofauti walipigwa hadi kuzirai na watu wanaodaiwa kushiriki kuchimba kaburi kwa
ajili ya kumzika marehemu Hussein.
Silwimba
alisema Hussein alifariki dunia Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuugua kwa muda
mrefu, lakini inaonekana kuwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walihusisha
ugonjwa huo ambao ulisababisha kifo chake na ushirikina.
Jana
mchana, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Momba aliyefahamika kwa jina la Wendo
aliongoza operesheni ya kufukua kaburi walimozikwa watu hao, ambao walikutwa
wakiwa wameshafariki dunia.
Silwimba
alisema miili ya Molela na Nachela ilifanyiwa uchunguzi, kisha kukabidhiwa kwa
ndugu na jamaa zao ambao waliifanyia mazishi jana mchana.
Mkasa wenyewe
Kundi la vijana tisa ambao wanadaiwa kuwa ndiyo waliokuwa wakichimba kaburi la marehemu Hussein walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu kwamba ni wachawi na kwamba walihusika na kifo chake.
Mkasa wenyewe
Kundi la vijana tisa ambao wanadaiwa kuwa ndiyo waliokuwa wakichimba kaburi la marehemu Hussein walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu kwamba ni wachawi na kwamba walihusika na kifo chake.
Silwimba
alisema katika harakati zao, walikwenda nyumbani kwa George Hussein ambaye ni
kaka wa marehemu lakini hawakumkuta, hivyo kuamua kuchoma moto nyumba yake kwa
kuwa walikuwa wakimtuhumu kuhusika na kifo hicho.
“Baada
ya kufanya uharibifu huo, walikwenda hadi nyumbani kwa Mzee Molela kisha
wakamkamata na kumpiga sana hadi hali yake ikawa mbaya kisha wakambeba hadi
eneo la maziko,” alisema na kuongeza:
“Waliporejea
kwenye msiba walimkuta Mama Nachela naye wakamkamata na kuanza kumpiga hadi
akazimia na yeye pamoja na Molela waliwavuta hadi kwenye kaburi ambako mazishi
ya Nongwa (Hussein) yalifanyika.”
Alisema
baada ya jeneza kushushwa kaburini, vijana hao wanaodaiwa kwamba walikuwa na
hasira walimvuta Molela na kumwamuru kuweka udongo kaburini, lakini alishindwa
kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya.
“Baada
ya kushindwa walimsukumiza kaburini na baadaye walimvuta yule mama (Nachela)
ambaye naye alikuwa hajitambui na kumtupa ndani ya kaburi halafu wakawafukia
wote, kisha wakaondoka,” alisema Kaimu Ofisa Mtendaji huyo.
Alisema
mwingine aliyekuwa akisakwa na vijana hao ni Fotino Sichilongwa na kwamba kabla
ya kufanya vitendo hivyo, vijana hao walimkamata Mwenyekiti wa Kitongoji,
Alfred Kukwe na kumfunga miguu na mikono kwa kutumia kamba, wakamlaza
kifudifudi, kisha kumnyang’anya simu yake ya kiganjani ili asiweze kutoa
taarifa kokote.
Alisema
Kukwe alifunguliwa kamba hizo saa saba na nusu mchana na ndipo alipopiga simu
sehemu mbalimbali kutoa taarifa za tukio hilo.
Silwimba
alisema baada ya taarifa hizo kusambaa kijijini Karungu, mwenyekiti wa kijiji
hicho na ofisa mtendaji wake, walikimbia na kwenda kujificha kusikojulikana
wakihofia kudhuriwa na vijana hao.
“Polisi
walipofika jana (juzi) jioni walikuta vijana wote waliohusika wamekimbia na
hawajulikani walipo maana nyumba zao zimefungwa, hili ni tatizo kubwa maana
limesababisha taharuki kubwa hapa kijijini,” alisema.
Wawili mbaroni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kulikuwa na taarifa kuwa Molela na Nachela wana undugu. Hata hivyo, habari kutoka kijijini Karungu zimesema hawana undugu wowote.
Wawili mbaroni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kulikuwa na taarifa kuwa Molela na Nachela wana undugu. Hata hivyo, habari kutoka kijijini Karungu zimesema hawana undugu wowote.
Kamanda
Diwani ambaye aliwashutumu wananchi kwa kujichukulia sheria mkononi, alisema
hadi sasa watu wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.“Tunawashikilia watu
wawili ambao tunaamini walikuwa vinara wa tukio hili la mauaji,” alisema
Diwani.
Kamanda huyo aliitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake waheshimu na kutii sheria bila shuruti na kuachana na imani za kishirikina.
“Kila
mmoja afanye mambo yake kwa kujiamini. Hii ya kuendekeza imani za kishirikina
ina madhara na zaidi ni kurudisha nyuma maendeleo. Jamii inatakiwa kutafuta
njia halali kufikisha kero na malalamiko badala ya kutumia vurugu na fujo na
kusababisha mauaji.”
No comments:
Post a Comment