Watu kutoka mji wa Wete Zanzibar wakinunua chakula sokoni. Bei za chakula zilipanda karibuni hadi kufikia asilimia 100 kutokana na kubadilikabadilika kwa bei za fedha za kigeni. |
Kubadilikabadilika
kukubwa kwa bei za chakula ambako Tanzania imeshuhudia katika miezi ya karibuni
ni ishara kwamba uchumi wa nchi haukutengamaa kimuundo, wanauchumi wasema.
Baada
ya bei za chakula kushuka kwa muda mfupi kutokana na kukaribia kwa msimu wa
mavuno wa mwezi Oktoba, zilipaa tena mwezi wa Novemba baada ya nchi kukumbwa na
uhaba wa mafuta.
Kwa
mujibu wa data zilizotolewa tarehe 23 Novemba na Wizara ya Viwanda na Biashara,
baadhi ya bei za mazao zilipanda hadi kufikia asilimia 100 katika wiki za
mwanzo za mwezi huu.
Kwa
mfano, mjini Dar es Salaam, bei kwa kila kilo moja ya maharage ilipanda kutoka
shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 1,200 (senti 75 za dola), bei ya
mahindi ilipanda kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 700
(senti 44 za dola), mchele kutoka shilingi 1,600 (dola 1) hadi shilingi 2,200
(dola 1.37) na unga wa ngano kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola ) hadi
shilingi 900 (senti 56 za dola).
Ili
kujilinda dhidi ya kuanguka kwa bei ya shilingi, Watanzania wengi wanategemea
dola ya Marekani na pesa nyengine za kigeni kwa ajilli ya kununua na kuuza
bidhaa, utaratibu ambao unazidisha kuiyumbisha pesa ya nchi na kusababisha
kupaa kwa bei za chakula, kwa mujibu wa Mushengezi Nyambele, mchumi na katibu
wa zamani wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
"Hata
watu wa kawaida wamepoteza imani na fedha yetu," aliiambia Sabahi.
"Wote wanachagua dola, jambo ambalo husababisha uhaba wa dola nchini, na
kwa hivyo kuchochea kuongezeka kwa bei." Alisema kuwa mafuta yanapanda kwa
sababu mzunguko mdogo wa dola nchini Tanzania, badala yake kuathiri bei za
bidhaa na huduma.
Nyambele
alisema kuwa kuyumba kwa sehemu kunatokana na kushindwa kwa sera za serikali za
fedha.
Matumizi
ya fedha za kigeni kwa biashara ya ndani ni haramu nchini Tanzania, lakini
serikali haijaweza kusimamia kwa ufanisi kuimarisha marufuku hiyo, Nyambele
alisema. "Ni rahisi kupata fedha za kigeni nchini Tanzania kuliko popote
ulimwenguni," alisema, na kuongeza kuwa dola za Marekani ni asilimia 95 ya
fedha zote za kigeni zinazotumika nchini.
Benki
ya Tanzania inapaswa kuzuia upatikanaji wa fedha za kigeni kwa wafanyabiashara
wa kimataifa na wasafiri kwa matumizi ya nje, alisema.
Mwezi
wa Julai, Waziri wa Fedha William Mgimwa aliliambia bunge kuwa serikali ilikuwa
na habari juu ya matumizi mabaya ya biashara za jamii na kuahidi kuwa serikali
ingefanyia kazi kuziba mianya.
Msemaji
wa serikali Assah Mwambene aliiambia Sabahi kuwa utawala inakamilisha mkakati
mpana wa kuondosha matumizi yasiyosimamiwa ya fedha za kigeni katika soko la
ndani, lakini akakataa kuweka wazi ni lini sera hiyo itaanza kufanya kazi.
Uhaba wa akiba ya nishati wazuwia uchumi
Pamoja
na hayo, ukosefu wa akiba imara ya nishati unasababisha changamoto kubwa zaidi
kwa uchumi kuliko matumizi haramu ya fedha za kigeni, kwa mujibu wa mwanauchumi
Honest Ngowi, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.
"Tunahitaji
kuupanua uchumi wetu na [kujenga] usalama wa nishati ili kujenga uchumi ulio
imara," aliiambia Sabahi. "Tunahitaji kuwa na mpango maalumu wa
vyanzo vya nishati ili kuepuka mifadhaiko ya nje."
Serikali
inapaswa kutumia kidogo zaidi na kutoa sera za kusimamia vizuri zaidi vyanzo
vya nishati na kujenga uchumi utakaoweza kufyonza mabadiliko ya masoko bila ya
kuathiri sana bei za walaji ambazo hulipia mitaani, Ngowi alisema.
Alisema
kuwa akiba ya mafuta ya Tanzania ni sawa na siku 15 za matumizi, ambayo
huufanya uchumi wa taifa kuwa katika hatari kwa mabadiliko ya masoko ya ndani
na ya kimataifa. "Tunahitaji kuweka malengo ya muda mrefu, kama vile kuwa
na mafuta ya kutosha ili kuusaidia uchumi wa nchi kwa muda wa miezi
minne," alisema.
Utulizaji
wa uchumi unaweza kufikiwa tu kwa kuweka sera za fedha ili kurahisisha
uwekezaji wa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na matangi makubwa ya akiba na
miundombinu mengine ili kusaidia vyanzo mbadala vya nishati, alisema.
No comments:
Post a Comment