WAFANYABIASHARA
watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali
Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala
mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza
katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola
moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni
(Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano
ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280
milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni – Dola 110 milioni).
Matajiri
hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao
katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima
wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.
Jarida
hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri
hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800
kutoka mataifa 17.
Asilimia
kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri
Afrika. Jarida
hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya
kuibuka na kuwa mabilionea.
SAID SALIM BAKHRESA
Jarida
hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana
uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.
Mfanyabiashara
huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake.
Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa
huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda cha usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea
kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye
kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream,
vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka
huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.
GULAM DEWJI
Mfanyabiashara
huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha
bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.
Alianza
na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni
kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.
Kampuni
hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya
petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.
Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.
“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.
ROSTAM AZIZ
Ameelezwa
kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo
kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.
Mwanasiasa
huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa
Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili. Aliachana
na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya
Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.
Ameelezwa
pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es
Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.
Akizungumzia
utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu
wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa
kwani ninamiliki asilimia 35.”
REGINALD MENGI
Mengi
anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda
vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.
Mfanyabiashara
huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya
biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.
Leo
hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali
ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa
Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za
IPP Gold na Handeni Gold.
ALI MUFURUKI
Utajiri
wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika. Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group. Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za
Afrika Kusini za Woolworth.
Infotech
hufanya kazi ya uendelezaji makazi na ukodishaji, matangazo na shughuli za
mawasiliano.
Ni
mmoja wa waanzilishi wa taasisi mbalimbali ikiwemo East Africa Capital
Partners, vyombo vya habari, sekta ya mawasiliano ikiwamo Venture Capital Fund
Manager na nyingine katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia
aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mwananchi Communications
Limited, Benki ya Stanbic, Mwenyekiti wa Africa Leadership Initiative East
Africa Foundation. Akizungumzia taarifa hiyo, Mufuruki aliwapongeza waliotajwa
kuwa ni matajiri.
“Ningefurahi
sana kama ningekuwa na utajiri huo lakini kwa upande wangu naona kwangu kuna
tatizo la taarifa kwani walizotoa si sawa,” alisema Mufuruki na kuongeza;
“Sizungumzii
watu wote waliotajwa, bali nazungumzia mimi mwenyewe ‘data’ walizotoa si sawa
kwa upande wangu.”
Hata
hivyo, alisema anafurahi kuona watu wanaanza kuzungumzia utajiri wa watu
wengine ‘in a positive way’ (kwa mrengo chanya) na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment