To Chat with me click here

Thursday, November 15, 2012

JK AMNG’OA MUKAMA, AMWEKA KINANA



AMTOSA CHILIGATI, AMWINGIZA NCHEMBA, ZAKIA MEGHJI, DK. ASHA-ROSE WAULA 


Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete

HAMATIYE Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameifumua na kuisuka upya Sekretarieti ya chama hicho, huku akimtupa nje Katibu Mkuu, Wilson Mukama.


Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemteua mwanasiasa mkongwe, Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya ambaye atakiongoza chama hicho kwa miaka mitano.

Kinana, ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, alikuwa meneja kampeni wa Rais Kikwete, hivi karibuni alitangaza kuachana na siasa kwa kile alichodai amekitumikia chama hicho muda mrefu.

Kutokana na uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mukama kuwa Mratibu wa Chuo cha Uongozi wa CCM pamoja na Vyama vya Ukombozi wa Bara la Afrika, kitakachojengwa katika eneo la Ihemi, mkoani Iringa.

Akitangaza uteuzi huo mjini Dodoma jana, Rais Kikwete alisema katika uteuzi huo ambao umeridhiwa na Halmashauri Kuu CCM (NEC), umekuwa na mafanikio kwa chama na Watanzania kwa ujumla.

Akiwataja walioteuliwa na kushika nafasi mpya, kuwa ni Vuai Ali Vuia, ambaye anaendelea na wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, huku Mwigulu Nchemba akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara.

Nchemba, amechukua nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na John Chiligati, ambaye ametupwa, wakati Mbunge wa Uzini, Dk. Mohamed Seif Khatibu, ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu, Oganizesheni akichukua nafasi ya Asha Abdallah Juma.

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Zakhia Meghji kuwa Katibu wa Halmshauri Kuu, Uchumi na Fedha.

Pia Rais amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-rose Migiro, kuchukua nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, nafasi ambayo awali ilikuwa inaongozwa na Naibu wa Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, huku Nape Nnauye akiendelea na nafasi yake Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi.

“Kwa kweli kikao hiki cha kwanza cha NEC, kimekuwa na mafanikio makubwa sana… kubwa hatua ya kukubalika kwa mapendekezo yangu mbele ya mkutano huu.

“Tumeunda Sekreterieti sasa, lakini suala la Kamati Kuu nimeiomba NEC kwanza iniachie, kuna wajumbe wengi wapya ambapo kama nitaiunda ninaweza kurudisha sura zile zile za wajumbe waliozoeleka.

“Lengo la kufanya hivi ni kuwafahamu, kwani kuna wajumbe wapya ili nao waweze kupata nafasi hii ambayo ni muhimu ndani ya chama chetu,” alisema Kikwete.

No comments:

Post a Comment