KATIBU
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema CCM watazunguka nchi nzima lakini
majibu yatajulikana 2015 kwani ndiyo utakuwa mwisho wao.
Pia Dk Slaa amesema Chadema hakiyumbishwi na kuahimia CCM kwa waliokuwa madiwani wake mkoani Arusha, na badala yake kinapata nguvu ya kuweza kusimamia maadili ya viongozi wake.
Pia Dk Slaa amesema Chadema hakiyumbishwi na kuahimia CCM kwa waliokuwa madiwani wake mkoani Arusha, na badala yake kinapata nguvu ya kuweza kusimamia maadili ya viongozi wake.
Dk
Slaa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu mambo
mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini, ikiwa ni siku moja tangu uongozi wa
juu wa CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana umalize ziara
yake ya kwanza katika Mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha.
Alisema
Chadema siku zote kitabaki kuwa mwalimu na vyama vingine vitafuata kwa kuiga
mambo ambayo chama hicho kimeyaanzisha. “CCM
kuzunguka huku na huko na ni kutuiga sisi kwani tumeanza muda mrefu, baada ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 tumekuwa tukizunguka na kuwaeleza wananchi mambo
mbalimbali,” alisema Dk Slaa na kuongeza;
“Wao (CCM) wazunguke tu lakini mambo yote yatajulikana 2015 kwani Watanzania wa sasa siyo wa kudanganywa tena.”
Dk
Slaa alisema anashangaa kwa nini CCM wanazunguka huku wakilalamika wakati wao
ndiyo wanaiongoza nchi hivyo majibu ya matatizo ya wananchi wanayo.“Chadema ni
mwalimu na wao hufuata, waendelee na mzunguko wao lakini waache kulalamika kama
sisi bali watoe majibu kwa kuwa wao ndiyo wanaongoza Serikali,”alisema Dk Slaa.
Akizungumzia
baadhi ya madiwani wa chama hicho waliohamia CCM, Dk Slaa alisema kuwa
hawakiyumbisha chama chao na kwamba hata kama wamehama wasipolipa Sh15 milioni
kama amri ya mahakama ilivyotolewa watakwenda jela.
Juzi
katika mkutano wa CCM Arusha, madiwani wa Chadema walitangaza kujiunga na CCM
huku wakipinga hatua ya Dk Slaa, kuwa alikuwa akitaka kuwafunga baada ya
kuwatimua ndani ya chama hicho.
Madiwani
hao ambao walitimuliwa na Chadema kutokana kitendo chao cha kumtambua Meya wa
Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo wa CCM ni Rehema Mohamed, Simba Salum wa Kata ya
Kati na Frank Joseph Takachi wa Kata ya Olasiti.
Jana
Dk Slaa alisema kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani kuna wanasiasa ambao ni
matapeli hapa nchini kwani madiwani hao walikwenda mahakamani kutaka
warudishiwe uanachama wao sasa wamekimbilia CCM. “Watanzania sasa wanajua
aina ya wanasiasa matapeli, kama walienda mahakamani kuomba uanachama
wanahangaika nini,”alisema Dk Slaa na kuongeza; “Chama hakitayumba na
tutaendelea kusimamia maadili ndani chama kama ilinavyotakiwa.” Alisema baadhi
ya madiwani wameshaanza kulipa fedha ambazo mahakama imesema, hivyo hao
waliokimbilia CCM wasipolipa fedha hizo ndani ya miezi miwili watakwenda jela
kama mahakama ilivyosema.
NCCR WANENA
Katika
hatua nyingine Chama cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM,
Tanzania Bara, Philip Mangula kushughulikia rushwa ndani ya chama hicho
kwa muda wa siku saba na siyo miezi sita kama alivyoahidi.
Kaimu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Faustin Sungura amesema vinginevyo chama hicho
kitawahamasisha wananchi waikatae CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Sungura alisema wahusika wa rushwa wanafahamika na
ametoa siku hizo kutokana na kuona miezi sita ni mingi na watendaji wa vitendo
hivyo wanafahamika katika chama na Serikali na kwamba kinachokosekana ni
dhamira ya dhati ya kuchagua viongozi wenye mikono safi
No comments:
Post a Comment