Baraza la mawaziri nchini Kenya
linapendekeza mabadiliko makubwa kwa sheria za ndoa nchini humo . Mswaada
wawaliowasilisha unapendekeza kuwa wanaume wanweza kuoa zaidi ya mke mmoja na
hata kuharamisha mahari ambapo familia ya mwanaume inalipa mahari hiyo.
Pia
inataka kuhalalisha watu kuishi pamoja kama mume na mke bila ya ndoa kwa
kipindi cha miezi sita kama njia ya kulinda watoto na wanwake wakati uhusiano
huo unapovunjika.
Mapendekezo
hayo tayari yamezua hisia kali kutoka kwa jamii kwa ujumla. Aidha mswaada huo,
lazima uidhinishwe na bunge kabla ya kufanywa sheria. Wengi
wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusianao kama huo
unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na
mume bila ya ndoa.
Wanafunzi
hujipata katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma
na punde baada ya kuhitimu , huvunja uhusiano ule. Mara
nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za manufaa ya ule uhusiano Wakati
mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo
ndipo mwanamue hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Na
hilo ndilo lengo la mswaada huu kulingana na baraza la mawaziri. Linasema
linataka ikiwa utakuwa sheria iweze kulinda akina mama na watoto kutokana na
dhulma za nyumbani hususan wanaume wanaokwepa majukumu yao. Mswaada
huu umevutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni
na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo
unapendekeza kutupiliwa mbali.
Dini
nyingi kama Uisilamu na hata wahindi wanakumbatia swala na mahari kwa sababu ni
matakwa ya dini. Ingawa
baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo, inaweza tu kuwa sheria ikiwa bunge
litaipitisha. Ikiwa kweli rekodi ya bunge hili ndio itakuwa kigezo cha
kupitishwa kwa mswaada huu, bunge lenyewe lenye asilimia hamsini ya wanaume,
litatupilia mbali mswaada huo au kuupitisha baada kufanya mabadiliko.
Wengi
wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusiano kama
huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na
mume bila ya ndoa. Wanafunzi
huishi katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma
na baada ya kusoma huachana.
Mara
nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za kujinufaisha kwa hali
yoyote ile. Wakati
mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo
ndipo mwanamume hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Mswaada
huu umvutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na
tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada
huo unapendekeza kutupiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment