To Chat with me click here
Showing posts with label Uchumi. Show all posts
Showing posts with label Uchumi. Show all posts

Thursday, November 14, 2013

KAGASHEKI ANASWA KONTENA LA PEMBE ZA NDOVU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amekamata kontena la futi 40 likiwa limesheheni pembe za ndovu kisiwani Unguja, Zanzibar jana alasiri.
Akizungumza na vyanzo vya habari hii kwa simu jana kutoka kisiwani humo, Waziri Kagasheki alisema kuwa kontena hilo lilikuwa likitokea Bandari ya Dar es Salaam na kwamba watu wawili wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi wakilisaidia Jeshi la Polisi.
Waziri Kagasheki alisema kuwa hadi sasa haijulikani mzigo huo una thamani kiasi gani na kwamba unasadikiwa kumilikiwa na raia wa China.
Alisema kuwa operesheni hiyo ni endelevu ili kuwabaini wahusika wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ya ujangili.
Tukio hilo linakuja zikiwa ni wiki mbili tangu waziri huyo kukamata pembe za ndovu 706 jijini Dar es Salaam zikimilikiwa na raia wa China.
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyamapori hapa nchini.
Wachina hao walikamatwa katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni wilayani Kinondoni chini ya operesheni iliyoongozwa na Waziri Kagasheki, ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.
 
Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China, ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung, ambao wamefikishwa mahakamani wiki iliyopita.

Wednesday, December 12, 2012

NEW TECHNOLOGY TO OFFER CLEAN WATER TO MILLIONS




A Tanzania government plan to supply 65 per cent of rural dwellers and 90 per cent of residents in urban areas with safe and clean water is likely to materialise, as a Japanese company is ready to chip in with simple, cost-effective and affordable water treatment technology.

The government drew up a nationwide water sector development programme five years ago in its quest to find a durable solution to the long-standing challenge of providing clean and safe water to over 44 million Tanzanians.

Essentially, the programme aimed at increasing people’s access to safe and clean drinking water for at least 90 per cent of urban dwellers and 65 per cent of those in rural areas.

Although some progress has been registered since the programme was commissioned, access to safe and clean water remains a big problem in many parts of Tanzania, and the situation is worse in rural settings, threatening the lives and health of millions.

A Japanese company, Poly-Glu Social Business Co. Ltd, has come up with new and affordable water treatment technology which could help Tanzanians cheaply access clean and safe water.

“I am going to Tanzania tomorrow (Tuesday) for the official launch of a pilot facility, just to demonstrate how this technology works,” said optimistic Dr Katetoshi Oda, chairman and chief executive officer of the company, which is trying to spread affordable water treatment technology to many poor countries where problems of safe and clean have reached crisis levels.

He told a team of journalists from developing countries who are on a two-week programme organised by the Japanese International Cooperation Agency (JICA) that the first water treatment plant would be installed in Bukoba.

With support from the Japanese government through JICA, the company has already successfully introduced the technology in some countries, including India, Somalia and Bangladesh.

In places districts and villages across Tanzania where the water treatment plants would be installed, local people would be given the opportunity to administer and operate the facilities, thus creating jobs for the people and increasing their income to meet other basic needs, he noted.

“Also, we would like the local people to develop new types of equipment from the original one. We want to empower the locals to be more innovative and creative, and design similar equipment instead of just imposing the technology,” said Oda.

Despite some failures in the implementation of the water sector development programme, the government is still committed to achieving universal access to safe and water as specified in the country’s Development Vision 2025 and Millennium Development Goal 7.

“We need to remain optimistic but at the same time be realistic with our ambitions,” The Guardian quoted the Minister of Water Prof Jumanne Maghembe as saying recently at the opening of the seventh joint water sector review meeting.

JET YAFICHUA MATUMIZI MABAYA YA ARDHI KILWA




Uwazi katika mikataba ya ardhi utawezesha kuondoa migogoro kati ya wawekezaji na wamiliki zikiwemo serikali za vijiji.

Hayo yameibuliwa wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea wilaya za Kilwa na Rufiji kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa matumizi ya ardhi, hususan katika uwekezaji katika kuzalisha nishati mimea.

Ziara hiyo iliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (Jet), ilifanyika katika vijiji vya Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti (Kilwa) na Rungungu, Mangwi na Chumbi C wilayani Rufiji.

Mwenyekiti wa Jet, Johnson Mbwambo, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa wimbi la uwekezaji mkubwa katika nishati mimea, limewaacha wanavijiji hao bila ardhi iliyotumika awali kwa kilimo na shughuli za maendeleo.

“Wanavijiji wengi hawana ardhi baada ya serikali kuingia mikataba na wawekezaji kukodisha ardhi kwa miaka mingi bila kujua masharti wala kuelimishwa na halmashauri za wilaya husika,” alisema.

Mbwambo alisema katika vijiji vya Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti, wanavijiji walidai kushinikizwa na viongozi wa wilaya na mkoa, kukodisha jumla ya ekari 160,000 kwa mwekezaji mmoja ambaye hata hivyo hivi sasa hajulikani alipo.

“Wanavijiji hao walidai kuwa mwanasheria wa mkoa, alisimamia mikataba hiyo kati ya mwaka 2006 na 2007 iliyoandikwa kwa Kiingereza pasipo kufafanulia haki na wajibu wao,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwambo, madai ya wanavijiji hao yaliungwa mkono na viongozi wao waliothibitisha kutokuwa na nakala za mikataba husika.

Pia walisema jitihada za kuzifuatilia nakala hizo ofisi za halmashauri ya wilaya na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) jijini Dar es Salaam, hazijafanikiwa.

Mbwambo alimnukuu Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa, Godfrey Jafar, akithibitisha ofisi yake kutokuwa na nakala ya mkataba wa ukodishwaji wa ardhi hiyo.

Ilielezwa kuwa kutoonekana kwa mikataba hiyo kumejenga hisia ya kuwapo mabadiliko, hasa yanayohusu muda wa umiliki. Mbwambo alisema uchunguzi uliofanywa na Jet ulibaini kuwa eneo hilo lililokodishwa kwa ajili ya kilimo cha miboni, halikutumika ilivyokusudiwa badala yake wawekezaji walikata miti, kutengeneza mbao na kuzisafirisha nje ya nchi.

“Baadaye alisitisha shughuli zote na maofisa wake kuondoka wilayani Kilwa kwa sababu ya kile kilichoelezwa iliishiwa fedha kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi duniani, alisema.

Aliongeza: “Kwa maana hiyo eneo hilo halijaendelezwa na vijiji havina haki kisheria ya kulitumia.”

Mbwambo alisema wanavijiji hao walipendekeza mambo kadhaa, ikiwamo kuitaka halmashauri za wilaya kuwajibika katika kuwaelimisha kuhusu masuala ya ardhi na mipata yake.

Pia walipendekeza kuondolewa kwa sheria inayowaruhusu wawekezaji kukodishwa ardhi kwa miaka 99, badala yake (ardhi) itumike kwa ubia na wamiliki (kijiji) kwa kipindi kisichozidi miaka 15.

Thursday, November 29, 2012

PESA ZA KIGENI, UPUNGUFU WA NISHATI VYAYUMBISHA SHILINGI YA TANZANIA


Watu kutoka mji wa Wete Zanzibar wakinunua chakula sokoni. Bei za chakula zilipanda karibuni hadi kufikia asilimia 100 kutokana na kubadilikabadilika kwa bei za fedha za kigeni.
Kubadilikabadilika kukubwa kwa bei za chakula ambako Tanzania imeshuhudia katika miezi ya karibuni ni ishara kwamba uchumi wa nchi haukutengamaa kimuundo, wanauchumi wasema. 

Baada ya bei za chakula kushuka kwa muda mfupi kutokana na kukaribia kwa msimu wa mavuno wa mwezi Oktoba, zilipaa tena mwezi wa Novemba baada ya nchi kukumbwa na uhaba wa mafuta. 

Kwa mujibu wa data zilizotolewa tarehe 23 Novemba na Wizara ya Viwanda na Biashara, baadhi ya bei za mazao zilipanda hadi kufikia asilimia 100 katika wiki za mwanzo za mwezi huu. 

Kwa mfano, mjini Dar es Salaam, bei kwa kila kilo moja ya maharage ilipanda kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 1,200 (senti 75 za dola), bei ya mahindi ilipanda kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 700 (senti 44 za dola), mchele kutoka shilingi 1,600 (dola 1) hadi shilingi 2,200 (dola 1.37) na unga wa ngano kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola ) hadi shilingi 900 (senti 56 za dola). 

Ili kujilinda dhidi ya kuanguka kwa bei ya shilingi, Watanzania wengi wanategemea dola ya Marekani na pesa nyengine za kigeni kwa ajilli ya kununua na kuuza bidhaa, utaratibu ambao unazidisha kuiyumbisha pesa ya nchi na kusababisha kupaa kwa bei za chakula, kwa mujibu wa Mushengezi Nyambele, mchumi na katibu wa zamani wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania. 

"Hata watu wa kawaida wamepoteza imani na fedha yetu," aliiambia Sabahi. "Wote wanachagua dola, jambo ambalo husababisha uhaba wa dola nchini, na kwa hivyo kuchochea kuongezeka kwa bei." Alisema kuwa mafuta yanapanda kwa sababu mzunguko mdogo wa dola nchini Tanzania, badala yake kuathiri bei za bidhaa na huduma.

Nyambele alisema kuwa kuyumba kwa sehemu kunatokana na kushindwa kwa sera za serikali za fedha.

Matumizi ya fedha za kigeni kwa biashara ya ndani ni haramu nchini Tanzania, lakini serikali haijaweza kusimamia kwa ufanisi kuimarisha marufuku hiyo, Nyambele alisema. "Ni rahisi kupata fedha za kigeni nchini Tanzania kuliko popote ulimwenguni," alisema, na kuongeza kuwa dola za Marekani ni asilimia 95 ya fedha zote za kigeni zinazotumika nchini.

Benki ya Tanzania inapaswa kuzuia upatikanaji wa fedha za kigeni kwa wafanyabiashara wa kimataifa na wasafiri kwa matumizi ya nje, alisema.
Mwezi wa Julai, Waziri wa Fedha William Mgimwa aliliambia bunge kuwa serikali ilikuwa na habari juu ya matumizi mabaya ya biashara za jamii na kuahidi kuwa serikali ingefanyia kazi kuziba mianya. 

Msemaji wa serikali Assah Mwambene aliiambia Sabahi kuwa utawala inakamilisha mkakati mpana wa kuondosha matumizi yasiyosimamiwa ya fedha za kigeni katika soko la ndani, lakini akakataa kuweka wazi ni lini sera hiyo itaanza kufanya kazi.

Uhaba wa akiba ya nishati wazuwia uchumi

Pamoja na hayo, ukosefu wa akiba imara ya nishati unasababisha changamoto kubwa zaidi kwa uchumi kuliko matumizi haramu ya fedha za kigeni, kwa mujibu wa mwanauchumi Honest Ngowi, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.

"Tunahitaji kuupanua uchumi wetu na [kujenga] usalama wa nishati ili kujenga uchumi ulio imara," aliiambia Sabahi. "Tunahitaji kuwa na mpango maalumu wa vyanzo vya nishati ili kuepuka mifadhaiko ya nje." 

Serikali inapaswa kutumia kidogo zaidi na kutoa sera za kusimamia vizuri zaidi vyanzo vya nishati na kujenga uchumi utakaoweza kufyonza mabadiliko ya masoko bila ya kuathiri sana bei za walaji ambazo hulipia mitaani, Ngowi alisema.

Alisema kuwa akiba ya mafuta ya Tanzania ni sawa na siku 15 za matumizi, ambayo huufanya uchumi wa taifa kuwa katika hatari kwa mabadiliko ya masoko ya ndani na ya kimataifa. "Tunahitaji kuweka malengo ya muda mrefu, kama vile kuwa na mafuta ya kutosha ili kuusaidia uchumi wa nchi kwa muda wa miezi minne," alisema.

Utulizaji wa uchumi unaweza kufikiwa tu kwa kuweka sera za fedha ili kurahisisha uwekezaji wa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na matangi makubwa ya akiba na miundombinu mengine ili kusaidia vyanzo mbadala vya nishati, alisema.