********************************
SIKU CHACHE ZILIZOPITA (IJUMAA) NILI-PUBLISH HABARI KWENYE BLOG HII, NIKIWATAARIFU KUWA, KAMANDA MWENZETU RAMADHANI MGAYA ALIPATWA NA HABARI ZA KUSTUSHA BAADA YA KUPOKEA SIMU TOKA MOROGORO KUWA BABA YAKE MZAZI ALIPATA AJALI YA GARI, AKIWA ANATOKEA IFAKARA KWENDA MOROGORO MJINI.
NAPENDA KUWATAARIFU KUWA HALI YA MZEE MGAYA INAENDELEA VIZURI KUTOKANA NA HABARI AMBAZO NIZIPATA NA KUTHIBITISHWA NA JAMAA WA KARIBU WA KAMANDA RAMA MGAYA. TUNAENDELEA KUMWOMBEA MZEE WETU HUYO APATE NAFUU YA HARAKA ZAIDI, ILI AWEZE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA KIJAMII.
LAKINI KATIKA HALI YA KUSIKITISHA KABISA, HAPA JUZI (JUMAMOSI) KAMANDA MGAYA ALIPATA TAARIFA ZA KUSIKITISHA MNO BAADA YA KUPIGIWA SIMU KUTOKA TANGA, KUWA SHANGAZI YAKE AMEFARIKI DUNIA (SIKUWEZA KUJUA MARA MOJA CHANZO CHA KIFO HICHO). HIVYO KUTOKANA NA HALI HIYO, ILIMLAZIMU KAMANDA MGAYA KUSAFIRI SIKU YA JUMAPILI KWENDA KUSHIRIKI MAZIKO YA SHANGAZI YAKE HUYO HUKO TANGA.
KWAKWELI KWA HALI YA KAWAIDA HALI HII INASIKITISHA NA KUTIA HUZUNI MNO. LAKINI KWA KUWA SOTE (WAISLAMU KWA WAKRISTO) TUNAISHI KWA NGUVU ZA MUNGU/ALLAH PEKEE. BASI NAAMINI MUNGU ATAMTIA NGUVU NA KUMWONGOZA VYEMA KAMANDA MGAYA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
SISI KAMA MAKAMANDA WENZAKE TUNAPENDA KUMTIA MOYO NA KUUNGANA NAYE KATIKA WAKATI HUU WA MAJONZI, AKUMBUKE KUWA MSIBA HUU UMETUSTUA NA KUTUGUSA SOTE (CHADEMA UKONGA). TUNAZIDI KUKUOMBEA WEWE PAMOJA NA FAMILIA YAKO ILI MFANIKISHE YOTE SALAMA NA MUNGU AWALINDE MRUDI SALAMA.
BWANA MUNGU ALITOA NA SASA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE.
No comments:
Post a Comment