Israil inasema imerusha
kombora nchini Syria, baada ya kituo chake kimoja cha jeshi katika milima ya
Golan kupigwa mzinga, ambao Israil inafikiri ni kutoka jeshi la Syria katika
mapambano yake na wapiganaji.
Tukio
hilo linakuja wakati makundi ya upinzani ya Syria, yanayokutana Qatar,
yametangaza kuwa yametia saini mkataba kimsingi kuwa na shirika moja litalokuwa
na serikali ya mpito, na kuwa ndilo linalopokea misaada kwa ajili ya maeneo
yanayodhibitiwa na wapiganaji.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Israil kushambulia jeshi la Syria, tangu vita vya
Mashariki ya Kati vya mwaka wa 1973.
Jeshi
la Israil limesema kombora moja lilirushwa dhidi ya Syria, baada ya kituo cha
Israil kwenye milima ya Golan kupigwa kwa mzinga.
Hakuna
mtu aliyeumia.
Mizinga
kadha ya Syria imeshawahi kuangukia upande wa Israil; na waIsraili walisema
kuwa watajibu iwapo itatokea tena.
Ni
wazi kuwa vita vya Syria vinafurika katika nchi za jirani. Huku
nyuma, upinzani umetangaza kwenye mkutano wao mjini Doha, Qatar, kwamba
umekubaliana kimsingi kuunda uongozi wa mseto utaojumuisha makundi yote makubwa
yalioko ndani ya Syria na nje.
Mataifa
ya magharibi yameahidi kuwa yatatambua na kusaidia ushirika.
No comments:
Post a Comment