WANANCHI
Mbalimbali mkoani Mara wameilalamikia Serikali kwa kutowekeza katika elimu ya
juu katika mkoa huu wa Kihistoria hapa nchini.
Wakiongea
kwa Nyakati tofauti na mwandishi wa habari hii,wananchi hao walisema kuwa msimu
huu kwasasa ni msimu wa wanafunzi kumaliza Shahada zao na shahada za juu lakini
kwa Mkoa wa Mara hakuna kitu kama hicho kinachoonekana hapa.
Walisema
kuwa kutokuwepo kwa vyuo vinavyotoa elimu ya Juu hapa MKoani Mara husababisha
hata suala la Maendeleo linakuwa la kusuasua kutokana na eneo kubwa kutokuwa na
Wasomi wa kutosha.
“Kiukweli
hili ni tatizo la Serikali kwani mkoa huu hakuna chuo kinachotoa Elimu ya Juu
hivyo wasomi hakuna na kutokuwepo kwa Wasomi ni tabu maana Jamii itabaki katika
mawazo Mgando” alisema Mzee Magesa John mtumishi mstaafu.
Mzee
Magesa alisema kuwa Mikoa mingi Tanzania yenye vyuo vinavyotoa Elimu ya juu
imekuwa na Mwamko mkubwa wa Jamii katika suala la Maendeleo tofauti na hapa
Mara kwani hakuna chuo chochote ambacho kingeweza kuleta hata changamoto kwa
Wazazi kuona umuhimu wa Elimu kwa vijana wao.
Akimuunga
kuhusu Suala hilo Mwalimu Emanuel Ghati naye alisema kuwa ni kweli
kukosekana kwa Chuo kinachotoa shahada katika mkoa huu ni kuendelea kuwatenga
wana Mara katika suala la Elimu,Mwali Ghati alisema kuwa ingekuwa rahisi kwa
watu kujiendeleza wanapotoka Kazini kuliko ilivo hivi sasa ambapo watu wengi
wakipangwa Kikazi Mara hawapendi kufanya kazi mkoa kutokana na kutokuwa na
mambo mengi.
“Hii
ni kweli maana kuja kufanya kazi huku kunapelekea kupoteza fursa nyingi hasa
suala la elimu kwani Mkoa kama Mwanza umeendelea kwa sababu una Vyuo ambavyo
kwanza vimesababisha Muingiliano kuwa mkubwa lakini pia vimesaidia Mwamko
katika Jamii” alisema Mwl Ghati.
Naye
Juma Jambo akitolea mfano Chuo kikuu cha Dodoma kilivyojengwa haraka na kuanza
kutoa huduma alihoji inakuwa Serikali kupitia wizara ya Maendeleo ya
Jamii,jinsia na watoto inashindwa kupandisha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare
kitoe kiwango cha Digree.
Alisema
chuo cha Kikuu cha Arusha kilichopo si msaada wa wana Mara kwani hicho ni chuo
ambacho kipo katika kujenga faida na si kuwasaidia Watanzania,hivyo Basi Jambo
aliongeza kuwa anadhani ni muda muafaka kwa serikali kuona umuhimu wa
kupandisha chuo cha Buhare kutoa kiwango cha Digree.
No comments:
Post a Comment