To Chat with me click here

Monday, November 26, 2012

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAPATA WASIWASI KUHUSIANA NA VURUGU KABLA YA UCHAGUZI WA KENYA






Timu ya ufuatiliaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetahadharisha kwamba migogoro inayoendelea nchini Kenya ingeweza kuathiri uchaguzi mkuu wa tarehe 4 Machi, 2013, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Jumamosi (tarehe 24 Novemba).

Katika ripoti yenye kichwa cha habari "Misheni ya Tathmini ya Kabla ya Uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki", EAC ilieleza kwamba machafuko ya huko Baragoi, huko Tana River Delta na Kisumu kunahitaji kushughulikiwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, kama masuala yaliyoibuliwa na kundi linalotaka kujitenga la Baraza la Jamhuri ya Mombasa.

Ripoti ilisema kuwa serikali ya Kenya imetoa kipaumbele cha hali ya juu cha usalama katika maandalizi yake, iliongeza kwamba Kamati ya Usalama wa Taifa na Wilaya "ikishirikiana na taasisi nyingine za serikali zimekuwa na wajibu muhimu wa kufanya kuelekea kuhimiza uchaguzi wa amani".

Ingawa ripoti hiyo ilisema Kenya imepiga hatua kubwa kwa kufanya uchaguzi wa kusifika, bado kuna matatizo katika maeneo ya kanda za kisiasa, ambayo yanazuia ufikaji wa vyama vya kisiasa katika maeneo ya nchi, gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti. 

Ripoti ilikuja baada ya timu ya ufuatiliaji ya watu 30, iliyoongozwa na Badru Kigundu, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda, kukaa siku mbili nchini Kenya wiki uliopita kwa mwaliko kutoka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.

No comments:

Post a Comment