Kiongozi wa Kundi la M23, Generali Sultani Makenga |
Kiongozi wa kisiasa wa kundi la waasi la M23
yuko mjini Kampala kwa mkutano na wakuu wa majeshi kanda ya maziwa makuu. Msemaji
wa kundi hilo, aliambia BBC kuwa mkutano huo utaangazia ikiwa waasi hao
wataondoka katika mji wa Goma.
Waasi
waliuteka mji huo, wiki jana, ingawa serikali ya Congo pamoja na nchi zingine
za ukanda huo zimewasihi waasi hao kuondoka katika mji huo kama sharti la kusikilizwa
kwa matakwa yao.
Waasi
wa M23 ni wanajeshi walioasi jeshi la Congo mwezi Aprili , na wanasema kuwa
serikali imekataa kutimiza baadhi ya makubaliano waliyoafikia mwezi Machi mwaka
2009.
Uganda
imekuwa ikipatanisha waasi hao na serikali ya DRC tangu mwezi Agosti.
Mwandishi
wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa waasi hao wana hadi
mwishoni mwa leo kuondoka Goma. Hali ya usalama mjini Goma ni tete huku
maelfu wakitoroka mwakao Hii
ndio amri iliyotolewa na viongozi wa kikanda siku ya Jumamosi.
Majirani
wa Congo, wakiongozwa na Uganda wanajaribu kuzima uasi huo Mashariki mwa nchi.
Kufuatia mkutano uliofanyika mwishoni mwa Juma, viongozi wa maziwa makuu
waliwasihi waasi hao kundoka Goma kabla ya kuanza kwa mazungumzo nao.
Rais
Joseph Kabila, alikutana na waasi hao pia mwishoni mwa wiki lakini akasisitiza
kuwa mazungumzo hayajaanza.
Waasi
wanasema wangalia wanatathmini hatua za kuchukua. Hata
hivyo jeshi la Uganda lilikataa kuthibitisha ikiwa kiongozi huyo, Brigedia
Generali Sultani Makenga yuko mjini Kampala. Baraza
la usalama la umoja wa Mataifa lilimwekea vikwazo vya usafiri wiki mbili
zilizopita kwa sababu ya harakati za waasi hao Mashariki mwa Congo.
No comments:
Post a Comment