Wachimbaji wadogo wadogo wa Almasi Zimbabwe |
Almasi zenye thamani ya dola bilioni
1.25 zimeibwa nchini Zimbabwe. Kulingana na shirika la Partnership Africa
Canada (PAC) Shirika hilo linasema kuwa huu ndio
wizi wa hali ya juu wa Almasi kuwahi kufanywa tangu enzi ya Muingereza Cecil
Rhodes aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri wa Almasi.
Shirika hilo linadai kuwa wizi huo
uliofanywa katika mgodi wa Almasi wa Marange, uliwanufaisha maafisa wa
Zimbabwe, wafanyakazi wa kimataifa wa madini na makundi ya wahalifu.
Afisaa mmoja katika sekta ya madini
nchini humo, alipuuza madai hayo akasema kuwa ni uongo mtupu. Ripoti ya shirika hilo ijulikanayo
kama, "Reap What You Sow'' ufisadi na uporaji katika mgodi wa Marange,
ilitolewa na shirika hilo la nchini Canada, ikinuiwa kwenda sambamba na mkutano
wa serikali kuhusu biashara ya Almasi.
Ukiukwaji mkubwa wa sheria.
Rais Robert Mugabe, katika hotuba yake
kwa wajumbe alisema kuwa serikali itazingatia sana sheria za kimataifa kuhusu
uchimbaji wa Almasi , uhifadhi na uuzaji wake. Almasi huishia kutengeza pete kama hizi
ingawa wanaochimba wanaishi kwa umaskini mkubwa
Shirika la kimataifa la kuchunguza
biashara ya Almasi, (Kimberley Process,) iliondoa marufuku dhidi ya biashara
hiyo iliyokuwa imewekewa Zimbabwe mwaka 2011 baada ya kuungwa mkono na Marekani
pamoja na Muungano wa Ulaya.
Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2009, kufuatia
mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu katika mgodi wa Almasi wa
Marange pamoja na ripoti kuwa maafisa wa kijeshi walikuwa wanajinufaisha na
biashara haramu Shirika la PAC lilisema kuwa ukiukwaji
huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kutisha.
''Tunakadiria kuwa almasi za thamani ya
dola bilioni mbili ziliibwa tangu mwaka 2008'' shirika hilo liliongeza.
Mwezi Julai waziri wa fedha wa Zimbabwe
Tendai Biti alisema kuwa nchi hiyo inatarajiwa kupata dola milioni miasita kama
mapato ya kigeni kutokana na mauzo ya Almasi nje ya nchi lakini waliweza kupata
tu milioni arobaini na sita.
No comments:
Post a Comment