Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa |
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete, kuwataka makada wa chama hicho kujibu mapigo ya
wapinzani,akidai wanafanya kazi ya kueneza uongo na kupotosha wananchi, CHADEMA
imesema inamvutia pumzi kabla ya kumjibu.
Akihitimisha mkutano mkuu wa CCM mjini
Dodoma juzi usiku, Rais Kikwete aliwataka mawaziri na makada wa chama hicho
kufanya mikutano ya hadhara na kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za
wapinzani badala ya kutegemea nguvu za Jeshi la Polisi.
Huku akionekana kukasirishwa na kasi ya
CHADEMA, Rais Kikwete alimtaja wazi wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod
Slaa, kuwa aliwahi kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.
“Slaa aliita mkutano akasema mimi, mwanangu
Ridhiwani na Rostam Aziz tulikutana kwenye hoteli moja jijini Mwanza, huku
akijua siku aliyoitaja mi nilikuwa kusini nikiendelea na shughuli
zangu,”alisema.
Rais Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya
upinzani,watu wazima hovyo,wanasema uongo mbele wananchi na hata wakati
mwingine kwenye vyombo vya habari wakinukuu takwimu za uzushi.
Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo ya kueneza
uongo kwa wananchi,Dk.Slaa alicheka kisha akasema:“Tunawatafakari na
tutawajibu,ila siyo leo, wala hatuna haraka.
“Mimi kwa kweli sikusikiliza hotuba yake, na
hata mkutano wa CCM sijaufuatilia, ila kama Kikwete kasema hayo unayoniuliza,
basi tutamjibu kwa utaratibu rasmi wa chama, leo sisemi kitu.
“Sisi ni watu makini, tunaamini katika kile
tunachokisema wala wasipaniki, tutawajibu. Maana wanadhani tunapoteza muda kufuatilia mkutano
wao,nilimsikia hata Nape Nnauye akisema juzi kuwa anajua tumeacha kazi
tunawakodolea macho,”alisema.
Dk.Slaa alisema kauli ya Nape ambaye pia ni Katibu
wa Halmashauri Kuu(NEC),Itikadi na Uenezi wa CCM,inachekesha, kwani CCM ya wao
kuacha kazi zao na kuikodolea macho ilikuwa ya zamani si hii ya leo.
Katika kile kinachoonekana kama CHADEMA kuinyima
usingizi serikali na CCM,
Kikwete aliagiza mawaziri wote kujiwekea
utaratibu wa kila mmoja kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya serikali
katika vyombo vyote vya habari.
Alisema kwa vile viongozi wa chama na serikali
hawajibu taarifa za upotoshaji zinazotolewa na wapinzani, wananchi
wanapozisikia zikirudiwa rudiwa bila kukanushwa wanaziamini.
No comments:
Post a Comment