Tume
moja ya serikali ya Zanzibar imependekeza kushtakiwa kwa mmiliki wa meli na
maafisa wote wa bandari waliohusika na
ajali ya boti mwezi Julai iliyopoteza maisha ya watu 81 na kusababisha
zaidi ya 200 ambao bado hawajapatikana, liliripoti gazeti la Daily News la
Tanzania.
"Mapendekezo
yaliyomo kwenye ripoti yanajumuisha hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya
wale wote waliotajwa ndani yake," alisema Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar
na kiongozi wa tume hiyo, Abdulhakim Ameir Issa. "Tume pia imeishauri
serikali kupitia sheria za usalama baharini na kuimarisha idara ya uokozi na
udhibiti wa majanga."
Ripoti
ya tume hiyo ilitaja uzembe, ufanyaji kazi usio wa kitaalamu na kutowajibika
kama sababu kuu za ajali ya meli ya MV Star Gates, ambayo ilikuwa ya pili
kuzama ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Tume hiyo pia ilithibitisha kwamba
boti hiyo ilikuwa imebeba abiria 447, zaidi kabisa na idadi ya abiria 290
iliyotajwa katika orodha rasmi ya abiria.
Ripoti
hiyo pia ilitaka kufidiwa kwa kila mtu aliyehusika kwenye ajali hiyo, zikiwemo
familia za marehemu, wale waliojeruhiwa na wasiojeruhiwa kwa angalau shilingi
125,000 (dola 78) kila mwezi kwa miezi 80.
Boti ya MV Star Gates
ilizama karibu na Kisiwa cha Chumbe kiasi cha saa 7:50 mchana, kwa mujibu wa
Mwinyihaji Makame Mwadini, waziri wa dola katika ofisi ya rais na mwenyekiti wa
Baraza la Mpinduzi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment