MAELFU ya
waombolezaji jana walijitokeza kushiriki mazishi ya msanii Hussein Ramadhan
maarufu kwa jina la Sharo Milionea, huku mamia wakizirai baada ya kushindwa
kujizuia wakati mwili wake unawekwa kaburini.
Mwili wa msanii huyo ulizikwa jana kijijini kwake Lusanga wilayani Muheza saa 7 mchana, katika tukio lililomshirikisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Waombolezaji walianza kumiminika kijijini Lusanga tangu juzi jioni na idadi yao iliongezeka zaidi jana asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.Sala ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma ambaye baadaye aliamuru jeneza hilo kupelekwa makaburini, ambako waombolezaji kadhaa walipoteza fahamu.
20 wapelekwa hospitali
Miongoni
mwa matukio yaliyojitokeza katika msiba huo ni baadhi ya waombolezaji kupoteza
fahamu msibani.Matukio tofauti ya watu kuzirai yalitokea wakati mwili wa msanii
huyo ulipokuwa unapelekwa nyumbani kwao kijijini Lusanga ukitokea Hospitali
Teule ya Wilaya ambako ulihifadhiwa tangu alipopata ajali Jumatatu usiku na
wakati wa mazishi.
Miongoni
mwa waliopoteza fahamu katika msiba huo ni wasanii na waigizaji wa filamu
waliokuwa wakiigiza na Sharo Milionea wakati akiwa katika kundi la AL Riyam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MC wa shughuli hiyo, Steve Nyerere, zaidi ya watu 20 walipoteza fahamu katika msiba huo na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
DC Mgalu
aliwaomba waombolezaji kutokuwa na shaka juu ya waliopoteza fahamu kwa kuwa
madaktari maalumu walikuwa wameandaliwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuwapa
huduma.
Mwananchi lilifika katika hospitali Teule na kukuta waliokuwa wamepoteza fahamu, wengi wao wakiwa ni wasichana, wakipata huduma huku wengine wakiomba kupewa ruhusa ili wakahudhurie maziko.
JK atuma
rambirambi
Rais
Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Waziri wa Habari, Utamaduni na
Michezo, Dk Fenella Mukangara kutokana na vifo vya wasanii watatu vilivyotokea
hivi karibuni, kikiwamo cha Sharo Milionea.
Taarifa
iliyotolewa jana Dar es Salaam na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
ilisema kuwa Rais Kikwete ameshtushwa na vifo hivyo vya ghafla.
Wasanii hao ambao walifariki dunia katika mazingira tofauti ni Mwigizaji wa Kundi la Kaole, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Wasanii hao ambao walifariki dunia katika mazingira tofauti ni Mwigizaji wa Kundi la Kaole, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Mwili
wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana wa jan kabla ya kupelekwa
kwenye nyumba yake ya milele
|
Rafiki
mkubwa wa marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono na Msanii
wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema jana mchana, Muheza mkoani Tanga.
|
No comments:
Post a Comment