To Chat with me click here

Tuesday, November 13, 2012

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA INTERPOL KUSHIRIKIANA KATIKA ULINZI


Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye makao yake mjini Arusha na Interpol walikubaliana kuongeza ushirikiano wa usalama katika eneo hilo, liliripoti gazeti moja la Tanzania hapo Jumapili.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Interpol mjini Rome mwishoni mwa wiki, na wanatarajiwa hivi karibuni kusaini makubaliano yanayoelezea uhalisia wa ushirikiano huo.

"Huku maingiliano ya EAC yakiimarika na kutanuka, kukiwa na uhuru unaotokana na utekelezwaji wa Soko la Pamoja, madhara kama vile uhalifu wa kimataifa kama madawa ya kulevya, biashara haramu ya binadamu, bidhaa feki na uhalifu kwenye mitandao, miongoni mwa mingine, pia yanakuwa ya kisasa zaidi na lazima yakabiliwe kikamilifu," alisema Katibu Mkuu wa EAC Richard Sezibera.

Aliongeza kwamba ushirikiano na Interpol utakuwa jambo muhimu sana katika juhudi za amani na ulinzi za EAC.

No comments:

Post a Comment