Daraja
hili ndilo linaunganisha vijiji vya Lundamatwe katika Manispaa ya Iringa na
Wangama wilayani Iringa katika Mto Ruaha. Inaelezwa
kwamba, daraja hili lenye miaka zaidi ya 100 lilijengwa enzi za Wajerumani miaka ya 1890 na bado linatumika hata sasa.
Hata
hivyo, liko katika hali mbaya na halikidhi mahitaji ya wananchi. Kwa kifupi, ni
hatari kwa usalama wa wananchi kwa vile limekwishazeeka kiasi kwamba ukipita
linatingishika huku mbao zikionekana dhahiri kuchoka ingawa wananchi wanavuka
kwa miguu, baiskeli na hata pikipiki.
Haijulikani
kama mamlaka husika zinalitambua hili. Pengine zingeweza kuliboresha daraja
hilo na kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kuwa na mawasiliano ya uhakika ya
barabara tofauti na ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment