BARAZA LA VIJANA CHADEMA JIMBO LA UKONGA - BAVICHA, JUMAMOSI WALIFANYA MKUTANO WAO MKUU WA PILI AMBAO ULIKUWA NA LENGO LA KUTATHIMINI HALI YA UTENDAJI KAZI WA BARAZA HILO JIMBONI HAPA HALI KADHALIKA KUONA NI JINSI GANI WANAWEZA (BAVICHA) KUTOA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUTEKELEZA MAAZIMIO YA CHAMA NA JIMBO KATIKA KUONGEZA WINGI WA WABUNGE, MADIWANI PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA ILI KUWEZA KUFANIKISHA CHAMA CHAO KUTWAA DOLA IFIKAPO OCTOBER 2015 KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO.
VILEVILE MKUTANO HUO, ULIHUSIKA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA, ILI KUZIBA MAPENGO YA NGAZI MBALIMBALI ZA KIUONGOZI AMBAZO ZILIKUWA WAZI, KUTOKANA NA BAADHI YA VIONGOZI HAO KUHAMA MAKAZI, VYAMA NA WENGINE KUTOTIMIZA WAJIBU WAO KULINGANA NA KATIBA YA CHAMA.
BAADHI YA VIONGOZI WALIOCHAGULIWA WALIKUWA NI: FRANK TUBETH (KATIBU MKUU), HELEN JOHN (MWEKA HAZINA). PIA VIONGOZI WENGINE WALICHAGULIWA KATIKA KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA NI: MAXMILLIAN KATTIKIRO (MWENYEKITI), KICHAMBATI KICHAMBATI (KATIBU) PAMOJA NA WAJUMBE KATIKA KAMATI HIYO NI: HAMISI GEA, MARY NOVAT, JANE MWAMBEGULE, JOHN SIMBA, HUSSEIN ATHUMANI, MC SUMA, JANA KINYAWA NA RAMADHANI MGAYA.
MGENI RASMI KATIKA MKUTANO HUO ALIKUWA NI KATIBU MKUU WA JIMBO LA UKONGA AMBAYE ALIUFUNGUA NA KUKABIDHI MWENYEKITI WA BAVICHA NDG. FREDRICK KABATI KUONGOZA KIKAO HICHO.
Meza Kuu ambapo walikaa viongozi wa Bavicha Jimbo na Mgeni Rasmi Jumaa Mwaipopo (Katibu Mkuu Jimbo Ukonga).
Mwenyekiti Bavicha Kushoto, na Katibu Mwenezi wake kulia, waendesha kikao. |
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakiwa wanafuatilia kwa ukaribu.
Katibu Mkuu mpya wa Bavicha Jimbo ndg. Frank Tubeth akihojiwa na waandishi wa habari.
Kamanda Hamisi Gea, mjumbe wa kamati ya rasilimali Fedha akiongea na waandishi
Kamanda Kattikiro Junior (Mwenyekiti wa Kamati ya Rasirimali Fedha - Kulia) akifuatilia
mkutano huo
Kamanda Mary Novat, mjumbe wa kamati ya Fedha na Uchumi akiongea na waandishi
No comments:
Post a Comment