To Chat with me click here

Monday, June 4, 2012

CHADEMA UKONGA YAENDELA KUIBOMOA NGOME YA CCM – JIMBONI


Meza Kuu ambapo waheshimiwa walikuwa wameketi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilendeleza wimbi la kuibomolea mbali na kuivunja vunja ngoma ya Chama cha Mapinduzi jimboni Ukonga kwa kile walichokiita kama mwendelezo wa mikutano ya hadhara ya kukijenga chama, ambapo wanachama wa CCM wameendelea kukihama chama chao kwa kuzisalimisha kadi zao za uanachama wa CCM kwa aliyekuwa akihutubia mkutano huo wa hadhara Mhe. Mabele Marando. Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mpira wa miguu maeneo ya Pugu Kajiungeni, ikiwa ni mwendelezo wa kunadi sera zake na kujenga chama zaidi ngazi ya Jimbo.

Akihutubia mkutano huo ambao ulihudhuriwa na mamia ya wananchi wa kata ya pugu na maeneo jirani, Mhe. Marando alisema kuwa, nchi imekuwa ikiendeshwa pasipo kufuata taratibu, kanuni na sheria za utawala bora, ambapo alisisitiza kuwa hali ngumu ya kimaisha pamoja na mfuko wa bei za juu za bidhaa ambazo hutumika na wannchi ni matokeo ya utawala mbovu wa chama tawala na serikali yake kwa ujumla. “Gharama na ongezeko la mfuko wa bei ni matokeo ya utawala mbovu wa CCM, unaponunua chochote kile kwa bei ya juu ni sababu ya chama tawala (CCM), alinukuliwa na vyanzo vyetu vya habari alipokuwa akihutubia.
Mhe. Marando akisalimiana na Baadhi ya wananchi kata ya Pugu baada ya kumaliza kuhutubia

 Vilevile alipokuwa akijibu baadhi ya hoja na maswali toka kwa wannchi alisema; Chadema imejiandaa vyema kuchukua madaraka na ndiyo maana pamekuwa na ongezeko kubwa la wanachama wanaohamia katika chama hicho hususani kutoka CCM, kwani wamekuwa na imani zaidi na CHADEMA kulinganisha na CCM. Pia akinukuhu moja ya “quotes” za mwasisi wa Taifa hili hayati Mwl. Julius Nyerere kuwa; “Hakuina chama makini na mbadala wa CCM kama Chadema” alisema kuwa, baba wa Taifa alikuwa akifanya ufunuo kuwa siku zinakuja ambapo Chadema itaisambaratisha CCM na hatimaye kuchuku madaraka kutokana na utekelezwaji mbovu wa sera zake. Akifananisha ufunuo huo na ule ulioko kwenye biblia wa Mt. Yohane ambapo alitabiri juu ya mambo yajayo katika kitabu hicho cha ufunuo wa Yohane. 

Mhe. Marando hakuishia hapo, alizidi kupigilia msumali wa moto pale alipowapokea makada wa CCM toka katika kata hiyo ya pugu ambapo baadhi ya wanachama wa CCM walikihama chama chao na kujiunga na Chadema rasmi. Wakiongozwa na aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo wanachama wengine wengi zaidi walizikabidhi kadi zao na kuunga mkona oparesheni ya Chadema ya "VUA GAMBA VAA GWANDA". 

Aliyekuwa Kaimu mwenyekiti wa CCM kata ya Pugu akionekana nadhifu katika T-shirt ya Chadema yenye ujumbe "Chadema Movement for Change - M4C"
 
Marando alisema kitendo cha wananchama hao wa CCM kukihama chama chao hadhani ni cha kishujaa na ndivyo kinatekeleza ufunuo wa baba wa Taifa kuwa CCM itavunjika vipande vipande, na ndivyo itokeavyo hivi sasa. Akidhibitisha madai hayo alisema mifano halisi ni jinsi tunavyoshuhudia migogoro kati ya wanachama na viongozi wa CCM wanavyolumbana na kutupiana maneno hadharani. Alitoa mfano kama vile Nape Nnauye ambaye ni katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM alivyokuwa akilumbana na Mhe. Maige ni wazi kuwa kuna mpasuko ndani ya CCM. 

Mbali na Mhe. Marando, mkutano huo wa hadhara ulihudhuriwa na watu wengine mashuhuli kama Mhe. Lucy Owenya, Katibu Mkuu wa Chadema-Jimbo pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA. Katika mkutano huo CHADEMA ilifanikiwa kuwapokea wanachama takribani zaidi ya kumi toka Chama Tawala (CCM) na wengine toka vyama vingine kama NCCR MAGEUZI.

Katibu Mkuu wa Chadema Jimbo la Ukonga Ndg. Mwaipopo akihutubia mkutuno huo kabla ya kuhitimisha. 
Akiongea na wananchi wa kata ya Pugu, katibu mkuu – Jimbo ndugu Mwaipopo, alisema kuwa baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa wakikipaka chama chake matope kwa kusema kuwa ni chama cha Ki-Kristo na Ukabila, akikanusha uvumi huo ndugu Mwaipopo alisema hayo ni uzushi wa watu wachache wasiokitakia mafanikio chama chake, na kuongeza kuwa, yeye mwenyewe ni muislam safi tena ni Ustaadhi, kisha kuhoji kama CHADEMA ni chama cha Ki-kristo imekuaje kwa yeye Ustadhi kuwa katibu wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama hicho? Hivyo aliwataka wananchi kutowasikiliza wazushi hao na kuungana pamoja wakihakikisha kuwa wanakijenga chama na kujiweka tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Moja wa wanachama wakongwe wa CCM akielekea kukabidhi kadi yake kwa Mhe. Marando kwa furaha kubwa.
Moja ya waaliyekuwa mwanachama wa NCCR - Mageuzi akijisajili na kupokea Kadi ya uanachama wa Chadema rasmi katika mkutano huo. 
"Mzee Karibu sana Chadema, Sisi sio mafisadi kama wao" Mhe. Marando akimkaribisha moja ya wanachama wapya wa Chadema (Mwenye Koti na Kofia) waliokihama chama cha mapinduzi hapo jana
Wananchi wa Kata ya Pugu wakifuatia kwa makini hotuba ya Mhe. Marando alipokua akihutubia viwanja hivyo vya Pugu Kajiungeni.
 Mwanachama mpya mwingine wa Chadema toka CCM akimkabidhi kadi yake ya CCM Mhe. Marando huku akisindikizwa na baadhi ya wafuasi watiifu wa Chadema.
Waheshimiwa walishindwa kujizuia kuendelea kukaa kwenye viti vyao baada ya kuona wana-ccm wanajisalimisha mbele yao kwa uongozi huo wa Chadema uliokuwa ukiendesha operasheni hiyo ya VUA GAMBA VAA GWANDA katika viwanja vya Pugu Kajiungeni.
Zilikuwa ni shagwe mno kwa wanachama pamoja na viongozi wa Chadema baada ya kuhakikisha wameibomoa CCM vilivyo katika maeneo hayo, kama waonekanavyo wakishangilia ushindi huo.
                                                                                

No comments:

Post a Comment