To Chat with me click here

Sunday, December 16, 2012

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI DK.EMMANUEL NCHIMBI ATANGAZA RASMI KUFUNGWA KWA KAMBI YA WAKIMBIZI YA MTABILA

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi
DECEMBER 11 mwaka huu zoezi la kuwarejesha kwao wakimbizi wa kambi ya Mtabila lilikamilika na kufanya idadi ya wakimbizi wote 35,357 kurejeshwa ispokuwa wakimbizi 1,540 tu ambao wako kwenye kambi ya Nyarugusu na hili ni kundi la 1993. 

Raia hao wa burundi awali8 walikua kwenye kambi ya Mtabila lakini kutokana na sababu mbalimbali walihamia kwenye kambi ya Nyarugusu ambayo wanaishi wakimbizi kutoka DRC bila ridhaa ya serikali na kusababisha kuvuliwa hadhi ya kuwa wakimbizi.


Tanzania hadi sasa inawakimbizi zaidi ya 60,000 kutoka nchini DRC, ambao inaendelea kuwahifadhi. Kufungwa kwa kambi hiyo inafanya idadi ya kambi za wakimbizi zilizofungwa kufikia idadi ya Tisa ambapo kabla ya kufungwa kambi ya Mtabila kambi zilizofungwa ni pamoja na, Karago, Mtendeli, Kanembwa na Nduta (Kibondo) Muyovosi (Kasulu) Kitali (Biharamulo) Lukole (Ngara) na Mkungwa Kibondo.

No comments:

Post a Comment