Papa Benedict XIV, akifungua akaunti ya Twitter |
Papa Benedict anafungua akaunti katika
mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa kanisa
katoliki.
Taarifa
kuhusu akaunti hiyo itatolewa baadaye hii leo katika mkutano na waandishi
habari, lakini duru kutoka Vatican zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe
kwenye akaunti hiyo.
Wanasema
Papa Benedict anapendelea kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.
Kanisa
hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni
limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.
Wakatoliki
kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo
itakapozinduliwa rasmi.
Papa
Benedict anataka kuitumia akaunti hiyo kuwasiliana na wakatoliki kote duniani.
No comments:
Post a Comment