To Chat with me click here

Monday, December 3, 2012

JENGO LA MAKUMBUSHO KUU ZANZIBAR LABOMOKA

Jengo la Makumbusho Kuu - Zanzibar
JENGO la Makumbusho Kuu ya Zanzibar, limebomoka upande wa Ngome Kongwe na kusababisha hasara kubwa ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye jana alitembelea eneo hilo kujionea uharibifu uliojitokeza.

Akiwa katika eneo la tukio, Maalim Seif ameuagiza uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuzuia matumizi ya jengo na kusisitiza kuwa, ipo haja ya kulifanyia matengenezo ili kutunza historia ya Zanzibar na hifadhi ya mji huo ambao ni urithi wa kimataifa.

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Bw. Said Ali Mbarouk, alisema jengo hilo limebokoka wakati likiendelea kufanyiwa ukarabati.

“Baada ya kuona athari zilizojitokeza awali, tuliamua kulifanyia ukarabati kwa kuanza uezekaji, lakini mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha jengo hili liendee kuvuja na kubomoka,” alisema.

Alisema kutokana na athari hiyo, wameamua kuitisha kikao ili
kutathmini hasara iliyopatikana ambapo baada ya kikao hicho watashirikiana na washirika wa maendeleo ukiwemo mradi wa MACEMP uliokuwa ukisaidia kukarabati jengo hilo na mengine
ya kihistoria ili waweze kuendelea na ukarabati.

Jengo la Makumbusho Kuu la Zanzibar ni miongoni mwa majengo muhimu ya kihistoria ikidaiwa hata umeme ulianza kuwaka katika kituo hicho katika eneo zima la Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment