To Chat with me click here

Wednesday, December 19, 2012

UTAJIRI WA KINANA NI TISHIO!!!!


Mhe. Abrahaman Kinana

KINANA TUONEE HURUMA WATANZANIA; HUU UJANGILI MKUBWA SANA, UNAUMA BILA KUPULIZIA? SWALI, UMEWEZAJE KUPATA UTAJIRI WOTE HUU? WIZI MTUPU... TUTASEMA SANA HADI WATANZANIA WAONE.....Endelea.....

Unajua Watanzania Tumezidi Ujinga sana, Yaani tunapelekwa pelekwa tu Kama misukule flani Na tunaridhika kabisa tu.. Jambazi, Mwizi wa Mali ya Umma, mdhulmati mkubwa, Bado anakumbatiwa tu Na watanzania tupo Na nchi ipo??!!? Tumekuwa zombie kiasi gani jamani..

Nchi HII ni Mali yetu sote jamani, Sio Kwamba nakuonea gere Kinana no!, Nchi sisi sote tuna haki nayo Hakuna mwenye hati Miliki Na Nchi hii..Lazima iwe Na Moyo wa Ubinaadamu Hata kidogo jamani, kila kitu umiliki wewe tu HE!! Mbona mlafi hivyo?

Msasani yoote Imejaa Majumba yako, mbali Na Jumba lako kubwa sana karibu Na CHUO Cha Tanesco mahando st lakini Bado Mwaya street imejaa majumba yako, mengine umepangisha makampuni , hivi Kwani nyumba moja haitoshi Kama kiongozi nyingine Na sisi tukajipatia???, bado una viwanja huko huko Msasani Hata hujavijenga hivi sisi turithi Nini mbona mnatuonea hivyo.

Sisemi Kwa Ubaya lakini Kwani kuchelewa kuzaliwa ndio zambi kubwa yetu kiasi tukose pahala pa kuishi?

Basi ni Heri Hata ungewapatia wanao wakae Kwenye majumba hayo lakini wapi, wanao watatu Samira, Hamza Na Yasin wote umeshawatoroshea Kanada, umeshawajengea huko wanakula bata Mwanzo-Mwisho, bado hatujaongelea Majumba yako huko Arusha anapokaa Yule Kaka yako uliyempiga uchizi, hapo Bado hatujaongelea Bandari yako ya Kuuza magari Temeke, Hapo Bado hatujaongelea Kampuni yako ya kufua nguo zote Za mahoteli makubwa FALCON, hapo bado hatujaongelea umiliki wako makumi ya makampuni hapa Tanzainia Na Meli zake, Hatupingi Mtu kuwa Bilionea this way lakini Kwa kiongozi wa Chama ni mfano gani tunapata..??!!

Hata Kama ukikasirika kuweka mambo yako nje mbona hapa sijaanika ndo naanza, kiongozi lazima uwe mwadilifu Na Mtu asiye Na Uchu Wa Mali this way..

Sasa watanzania tunasimamia rasilimali zetu, Na najua mimi Na wewe ni marafiki Wa Muda mrefu sana ila Mwenzangu dhambi sasa Basi umezidisha mno.. Achia Mali Za watanzania, usipokubali kusalimu amri Mbele ya Watanzania Basi ntakwenda press Conference Na Kutangaza karatasi Kwa Karatazi Ufirauni wako Woote. Kisha freely ntakuruhusu unifanye unachotaka kunifanya, si mmezoea kuua?!?Mie sio Kama Regnald Mengi, unamtisha kidogo anatetemeka, Nunua magazeti yote , Chimba biti Wahariri wakuu Wa magazeti yoote wasiandike habari zako lakini jua Mwisho umesika, Hutaweza, siku hizi kuna so many media to report madudu yenu..

Tuweni wazalendo jamani.. Tuweni wazalendo .. Mungu lazima aibarikia Ardhi yetu..
Kwa hisani ya Chadema Nguvu ya Umma!!!!

No comments:

Post a Comment