Ofisa wa trafiki akiongoza msongamano
wa dala dala kwenye barabara ya Uhuru katika eneo la Congo la Dar es Salaam.
|
Serikali
ya Tanzania kuanzia Jumamosi (tarehe 1 Disemba) itaacha kutoa leseni kwa
makampuni binafsi ambayo yanaendesha mabasi ya usafiri wa umma jijini Dar es
Salaam, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
ilitangaza.
Pia
serikali haitahuisha leseni zilizopo kwa magari binafsi ya usafiri, hata hivyo,
yataendelea kufanya kazi hadi vibali vyao vimalizike muda wa matumizi, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Ahmad Kilima.
Waendeshaji
wa mabasi ya usafiri wa umma ambao wanataka kufanya kazi kama makandarasi wa
serikali watapewa leseni za muda hadi mikataba itakapoanza kutumika mwezi Juni
2013.
Harakati
hii ni sehemu ya mpango mkubwa wa kubadilisha mabasi madogo na mfumo wa mabasi
ya umma yaendayo kasi unaosimamiwa na serikali. Serikali inategemea mpango wa
usafiri mpya kuboresha usafiri wa umma, ukipunguza msongamano wa magari Dar es
Salaam, ambapo SUMATRA inasema iliwagharimu Watanzania kiasi cha shilingi
bilioni 4 (dola milioni 2.5 ) kila siku, kwa kuwa wasafiri wanapoteza muda
mwingi kwenye msongomano wa magari.
Tangazo
la Jumatano (tarehe 28 Novemba) lilikuja mwezi mmoja baada ya serikali kuzindua
mfumo wa kwanza wa usafiri wa reli ya umma wa mji huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam Cosmas Tekule alisema usimamishaji
wa kutoa leseni kwa takribani magari madogo 10,000 ya usafiri wa umma,
yanayojulikana kama "dala dala", ulikuwa ni wa lazima kwa sababu
hayana uhakika na yanasababisha msongamano na uchafuzi.
"Tunaleta
mabasi makubwa ambayo yatabeba hadi abiria 150," aliiambia Sabahi.
"Kwa madaladala, yanayochukua abiria wapatao 30, unahitaji magari madogo
matano ya abiria kuingia katikati ya mji kuchukua idadi hiyohiyo ya watu. Ni
dhahiri, hii ni gharama kubwa."
Alisema
matumizi ya mafuta pia yatapungua kwa mabasi makubwa, kupunguza utoaji wa gesi
ya kaboni, ambalo ni jambo zuri kwa mazingira. Mabasi mapya yanatarajiwa
kuhudumia kiasi cha abiria 800,000 kila siku.
Zaidi
ya hayo, serikali inajenga upya barabara kadhaa na kuweka barabara ya magari
yaendayo kasi kwa mabasi mapya.
Pontian
Michael, mmiliki wa kampuni ya kuchomelea vyuma katikati ya jiji, aliiambia
Sabahi kwamba uondoaji kwa awamu wa daladala utaboresha maeneo ya maegesho
katika wilaya za biashara, ambayo alisema yamezuia wateja wanaotarajiwa.
MAANA YA HII KWA MADEREVA WA DALA DALA
Lakini
madereva walisema mfumo mpya wa usafiri wa umma utapelekea kupoteza kazi kwa
wengi miongoni mwao.
Mohamed
Ibrahim, ambaye amekuwa akiendesha katika jiji kwa miaka 22, alisema wamiliki
wengi wa mabasi ya usafiri wa umma ni wafanyabiashara wadogo ambao hawawezi
kushindana dhidi ya wafanya biashara wakubwa kupata mkataba na serikali.
"[Wamiliki wa makampuni makubwa] watawaajiri ndugu zao na karibia madereva
wote wa dala dala wataachwa bila kazi," aliiambia Sabahi.
Michael
Kakele, mmiliki wa dala dala anayesimamia Kampuni ya Kakele Transport, alisema
kwamba waendeshaji binafsi wamekuwa katika mazungumzo na serikali kuhusu
kipindi hiki cha mpito tangu mwaka 2010, na wanafurahia kufanya kazi katika
muundo huu mpya.
Lakini
aliiambia Sabahi itakuwa vigumu kumudu gharama za ununuzi wa mabasi ambayo yatafikia
viwango vipya, kwani yatagharimu hadi shilingi milioni 250 (dola 160,000),
ambazo wamiliki hawawezi kukopa kirahisi katika benki. Serikali inaweza
kuwasaidia wamiliki kupata mabasi na kupata sifa za mikataba kama itatoa
dhamana ya mkopo kwa angalau wale wanaoendesha usafiri wa umma ambao walikuwa
katika biashara kwa muda mrefu, alisema Kakele.
No comments:
Post a Comment