To Chat with me click here

Tuesday, December 4, 2012

WAKAZI WA YOMBO VITUKA WATOA MAONI JUU YA KATIBA MPYA

Jumapili iliyopita wakazi wa Yombo Vituka walipata nafasi ya kutoa maoni yao kwa tume ya katiba juu ya katiba mpya inayotarajiwa kuundwa hivi karibuni. Wadau mbalimbali walishiriki katika kutoa maoni yao ambao wengi wao walieleza zaidi juu ya kupunguzwa kwa mamlaka ya rais. 

Meza ya watumishi wa tume wakiwa wanafuatilia kwa makini michango ya wananchi. 
Baadhi ya wakaazi wa Yombo Vituka wakitoa maoni yao kwa tume ya katiba. 
Mwenyekiti wa Kikao hicho akihitimisha mkutano huo wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya huko Yombo Vituka.
 Magari ya Tume ya katiba yakiwa yameegeshwa kando kando ya viwanja vya ofisa ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Yombo Vituka, huku maoni ya wananchi yakiendelea kukusanywa. 

Kwa Wananchi Wote:
Maxmillian Kattikiro Blog inapenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wananchi wote kuwa, muda wa kutoa maoni juu ya katiba mpya bado haujaisha, hivyo kila mtu anaalikwa kuendelea kutoa maoni yake juu ya katiba mpya, kwani ni haki ya kila mwananchi kushiriki/kushirikishwa katika mchakato mzima wa kuundwa kwa katiba mpya. 

Kama haukupata nafasi ya kutoa maoni juu ya katiba mpya wakati kamati ya kukusanya maoni ilipopita katika maeneo yako, Maxmillian Kattikiro Blog, tunakukumbusha kuwa bado unaweza kuendelea kutoa maoni kwa njia zifuatazo;- 

1. Kwa njia ya barua pepe (e-mail): katibu@katiba.go.tz 

2. Kwa barua za posta, kwa anuani ifuatayo: 
    S. L. P. 1681, Dar-Es-Salaam, Tanzania. 

3. Maoni katika tovuti ya kamati ya katiba mpya. Fuata link hii hapa ili kutoa maoni yako; 

Hakikisha unashiriki, ni haki ya kila mwananchi (wale waishio  nnchi/hata nchi za nje). Pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli, na maendeleo katika nchi yetu kwa kutoa michango mihimu ambayo itakuwa ni mwongozo wa uwajibikaji kwa wote walio na dhamana ya kuwatumikia wananchi.

No comments:

Post a Comment