President Robert Mugabe - Zimbabwe. |
HARARE,
Zimbabwe
MFANYAKAZI
za ndani ‘hausigeli’ amehukumiwa kifungo cha miezi miwili jela na viboko, kwa
kosa la kumnywesha mkojo bosi wake kutokana na hasira ya kutolipwa mshahara
wake kwa wakati.
Rita
Chakwesha mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliajiriwa katika nyumba iliyopo
kwenye Barabara ya Avenue mjini Harare, kwa makusudi alimnywesha mwajiri wake
Sharlotte Chivavarirwa maji yaliyokuwa na mkojo ndani yake.
Chakwesha
alionekana mbele ya Hakimu Barbra Masinire huko Harare, akihukumiwa kwa makosa
hayo, huku akijitetea kuwa alikuwa akifanya hivyo kutokana na kutopewa ujira
wake kwa miezi miwili.
Mshauri wa
Jimbo la Francesca Mukumbiri aliiambia mahakama kuwa Novemba 5 majira ya saa 11
jioni, Chivavarirwa alirejea nyumbani akitokea kazini, na mara baada ya kufika
alimwomba msichana wake wa kazi Chakwesha ampe maji kutoka katika jokofu.
Chakwesha alienda na kumiminia maji ambayo tayari alikuwa ameyatia mkojo na kumpa bosi wake kwamba ayafurahie kwani ni maji yaliyokuwa na ladha nzuri.
Mama huyo
mwenye nyumba baada ya kufungua jokofu aliona glasi yenye kitu chenye rangi ya
manjano na harufu mbaya, hivyo akahisi kuwa huenda ni mkojo.
Hata hivyo, Chakwesha hakuishia hapo, alijikuta akitoa siri kwa rafiki wa karibu na Chivavarirwa, ambaye hakutaka kuitunza siri ile.
Rafiki huyo
alikwenda kumweleza hali halisi Chivavarirwa ambaye aliamua kulipeleka suala
hilo chini ya sheria na hivyo Chakwesha alikamatwa.
Kabla ya
kuburutwa mahakamani, Chakwesha alikiri kutenda kitendo hicho cha ajabu na
kwamba hali hiyo ilitokana na mwajiri wake kutomlipa ujira wake “Ndanga
ndabatwa nemweya wehutsinye,” Chakwesha aliiambia mahakama.
No comments:
Post a Comment